Habari mpendwa msomaji wa BIDEISM BLOG. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama.
Leo ni siku Muhimu sana aliyotujalia Mungu na tukiiitumia vizuri itachangia kikubwa katika mafanikio yetu.
Najua umeshangaa kuona kichwa habari na kutaka kujua nimeandika nini hasa. Ni wazi pia maneno aliyotumika kwenye kichwa cha makala ya leo wala si maneno mageni kwako umekuwa ukiyasikia kwenye masikio yako walau kila siku. Kama hukuwahi kuyasikia basi ngoja nikwambie kwamba na maneno yanayosikika kwenye wimbo wa mwanmuziki Darasa unaoitwa ''MAISHA NA MUZIKI'', Juzi wakati naangali hotuba ya raisi akiwa mkoani Mtwara nimlimsikia raisi naye akiyatamka maneno hayo kama yalivyo bila kupindisha
.
Nisikupeleke nje ya mada, lakini maneno haya '' unataka kukimbia na hauna breki, what do you expect!!' yana maana gani?. baada ya kuyatafakari mimi binafsi kuna kitu nilijifunza. Ebu fikiria kwamba umepanda gari na halina breki na mnapita katika mlima kitonga au sekenke au ule wa kule kwetu Nyanyoye. Ipo wazi hakipona mtu hapo itakuwa ni ile kitu tunaita bahati ya mtende.
Sasa msemo huu, kwangu mimi unanifunza kujiandaa na kuanza mapema na wala si kukurupuka, mwanafunzi ambaye hajiandai vizuri na mitihani moja kwa moja lazima kwake kufeli ni kugusa tu,anakimbia bila breki, Abraham Lincoln aliwahi kusema '' nikipewa masaa matatu kukata mti, mawili nitayatumia kunoa shoka'', alitaka kutuonesha uzito wa kujiandaa, uwezo wa kufunga mikanda na kuweka breki sawa ili tusianguke, lakini pia tukumbuke ''Mvua ilikuwa hainyeshi NUHU alipoanza kuijenga safina''.
Kumbe hatuna budi kujipanga na kujiandaa katika kile tunachozamilai kufanya aju kutimiza katika ndoto zetu. chukulia timu kabla ya kuingia uwanjani kucheza uwa wanfanya ''warm up'' ili kuweka miili yao tayari kwa michezo, tena uwa wanamefanya mazoezi mengi siku za nyuma ikiwemo kawasoma maadui wao. Hawa ni mfano wa kujiandaa.
Watu wengine hasa vijana wanatamani kuwa na maisha bora lakini hawataki kujishighulisha, wanakaa tu vijiweni, weekend ni watu wa kula bata, Darasa aliwaimbia watu wa namna hiyo ''unataka kukimbia na hauna breki!!, what do you expect?''. lakini pia tajiri namba moja Afrika bwana ALIKO DANGOTE alwahi kusema ''Vijana wengi wanatamani kupata mafanikio ambayo niliyapat kwa zaidi ya miaka kumi na nane kwa usiku mmoja'' yaani leo alale maskini kesho, aamke tajiri. My dear ''Unataka kukimbia na hauna breki!, what do you expect?''. THINK BIG!
Ni mimi rafiki na ndugu yako.
EDIUS BIDE KATAMUGORA
T UWASILIANE:
0764145476
0625951842 (Tuma neno "SUBSCRIBE" kupitia WHATSAPP niwe nakutumia makala zangu moja kwa moja).
email; ekatamugora@gmail.com
"SEE YOU AT THE TOP".
Karibu tena katika blog yetu kusoma makala nzuri kama hizi. Usisite kuwashirikisha na wenzako.
Friday, 10 March 2017
Edius Katamugora
Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.
0 comments:
Post a Comment