Monday, 6 March 2017

Wazo Lako Ndio Mafanikio Yako.

Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu umeamka salama na umejiweka tayari katika kuyatimiza majukumu yako. Endelea kupambana na kuweka juhudi katika kile unachokifanya nakuhaidi utafanikiwa.

Karibu sana katika makala ya Leo inayosema "Wazo lako ndiyo mafanikio yako". Kuna wakati niliwahi kuandika ya kwamba kila kitu kimeanza na wazo. Nguo unazovaa ni mawazo ya watu. Simu unayotumia ni wazo la mtu na hata gari unalotumia lilianza kama wazo. Kumbe wazo limebeba kitu kikubwa katika mafanikio yetu. Nikaongeza ya kwamba hata uumbaji wetu ulianza kama wazo kwenye biblia tunasoma "Na tumfanye mtu kwa sura na mfano wetu".

Kumbe unapokuwa na wazo Fulani usikubali life, Fanya kila jitihada zozote uhakikishe likiendelea. Unapoamka amka na wazo lako kichwani, unapofanya kazi weka maanani wazo lako na hata unapokwenda kulala lala ukiota wazo lako.

Kwanza kabisa uzuri wa kuwa na wazo Fulani ni hatua kubwa sana ya ugunduzi. Katika karne hii ya ishirini na moja ambayo watu wengi wanakaulimbiu ya "hakuna jipya chini ya jua ". Kumbe unapokuwa na wazo tayari umeshaondoka na kundi kubwa la watu wa namna hiyo. Ninaposema wazo linaweza kuwa; wazo la biashara, unataka kufungua kampuni, unataka kuandika Kitabu, unataka ununue shamba kubwa uanze kilimo cha aina Fulani. Hayo yote ni mawazo na ukiyafanyia kazi nakuhakikishia tu lazima utafanikiwa.

Wazo la kumiliki kampuni ya "Microsoft" la bwana Bill Gates toka akiwa na umri wa miaka kumi na moja ndilo linalomfanya Leo awe tajiri namba moja duniani. Wapo watu wengi wa namna hiyo.

Kubali pia kuwaambia watu wazo lako,  usiogope hata likiibiwa kama ni wewe umelianzisha wazo I'll hata ukianza kulifanyia kazi unaweza kulifanya kwa uhodari wa hali ya juu kabisa.

Usikubali kukatishwa tamaa na watu mbalimbali. Mara nyingi tunapokuwa na wazo Fulani, watu wengi upenda kutukatisha tamaa zaidi ya kutupa hamasa. Tambua jambo hilo, watu hawa wanaweza kuwa, wazazi,ndugu,jamaa, watu wa karibu, rafiki wa karibu,mshauri wako wa kila siku, kutaja machache.

Bwana Nnandi Egeizbo mbaye ni raia wa Nigeria, ndiye mmiliki wa kampuni za SLOT,Infinix na Tecno. Wakati akiwa fundi kompyuta nchini kwao , aliwahi kupeleka wazo lake la kutengeneza simu yenye kutumia laini mbili kwenye kampuni ya NOKIA, wazo hilo lilipingwa vikali kwani kampuni ya Nokia ilikuwa ikiona fahari kwa mtu kutembea na simu mbili mkononi na pia walijua wakitengeneza simu za laini mbili watapoteza mauzo yao yaani yatapungua. Bwana Nnandi hakukata tamaa baadaye alienda China ambako alikutana na bwana mmoja ambaye alikuwa akifanya kazi kwenye kampuni ya BIRD na alienda nae Nigeria. Ndipo walipofanikiwa kutengeneza simu ya tecno ya kwanza kabisa T 201. Leo hii kampuni ya tecno nani asiyeijua?. Kila mahali unapotembea kati ya watu kumi, watano wanamiliki simu za tecno. Nokia waliokataa wazo leo hii ndio bidhaa zao zinapotea siku hadi siku.

"Wazo lako ndiyo mafanikio yako"

Ni Mimi rafiki na ndugu yako.
Edius Bide Katamugora.
Tuwasiliane;
0764145476
0625951842 (Tuma neno "SUBSCRIBE" niwe nakutumia makala zangu moja kwa moja)
Email; ekatamugora@gmail.com
Facebook page: bideismblog (usisite kulike page yetu)

"See you at the top"

Tangazo;
Nimeandika Kitabu kinachoitwa "Barabara Ya Mafanikio" unaweza kuweka oda yako mapema kwani nakala zitakuwa chache. Asante

Usisite kuwashirikisha wenzako kile unachojifunza hapa.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: