Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama siku ya Leo na umejiweka tayari kufanya kitu kipya kitakachokusaidia kutimiza ndoto zako.
Karibu sana kwenye Makala nzuri ya Leo niliyokuandalia. Leo nitazungumzia baadhi ya mambo muhimu ambayo kila mfanyabiashara na mjasiriamali anapaswa kuyafahamu. Usiache kusoma kwa sababu wewe si mfanyabiashara au mjasiriamali kwani leo hii kila kitu ni biashara hivyo unatakiwa uanze kujifunza taratibu.
Nisikuchoshe sana mambo haya ni kama yafuatayo;
Jitahidi kusoma Vitabu na magazeti ambayo kwayo unaweza kupata mawazo ya kuikuza biashara yako na pia kupata wazo linaloweza kukuletea pesa. Ndiyo maana nimekuandikia Kitabu kinachoitwa Barabara Ya Mafanikio, usikose nakala yako kwani kuna mengi ya kujifunza kama mfanyabiashara au mjasiriamali.
Biashara ni sawa na mashindano ya michezo mbalimbali ambapo unapaswa kumjua mshindani wako. Ukimjua mshindani wako katika biashara unayofanya itakusaidia usipoteze Wateja.
Tambua kwamba kila wazo ulilonalo wewe, kuna mtu katika pande yoyote ya dunia analifanyia kazi na anatamani lizidi hilo wazo lako kwa kiasi kikubwa.
Kumbuka pia kutumia kanuni ya 7 × 24 × 365 × siku zote. Nikimaanisha kila muda ulionao ni muda wa biashara. Hakuna mapumziko.
Siku zote endesha biashara zako kana kwamba unashindana na makampuni makubwa. Fikiria siku zote kwamba makampuni hayo yakianza kufanya biashara kama yako itakuwaje?, lazima yatakushinda hivo kujiandaa mapema ni muhimu. Hii itumie hata kwenye kipaji chako.
Tumia muda wako mwingi kuwasiliana na wateja wako kwani ndiyo wanaokuweka wewe kwenye biashara yako. Usitumie muda mwingi kuwasiliana na watu ambao hawana tija kwenye biashara zako.
Fanya bidii katika kila uwezalo ujifunze chochote kinachohusiana na biashara yako. Itumie vizuri intaneti kujifunza mambo mengi kuhusiana na biashara unayoifanya au unayotarajia kuifanya. Fanya urafiki na watu wanaofanya biashara kama yako. Watakusaidia kujifunza mambo mengi kuhusu biashara yako.
Unaposhindwa mahali Fulani jifunze kutokana na makosa. Kwenye biashara makosa ni sehemu ya shule.
See you at the top
Ndimi
Edius Bide Katamugora
Author & motivational Speaker
0764145476
0625951842 (whatsapp)
E-mail: ekatamugora@gmail.com
Karibu sana kuweka oda Kitabu cha Barabara Ya Mafanikio. Bei ni shilingi 10000/= tuwasiliane kwa mawasiliano hapo juu.
Usisite kuwashirikishe wenzako ulichojifunza. Karibu sana.
0 comments:
Post a Comment