Friday, 26 May 2017

Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba u mzima na umeamka salama siku ya Leo.
Ni jambo la busara kabisa kumshukuru Mungu kutupa siku njema kama ya Leo. Leo ni siku muhimu sana kwenye maisha yako usikubali  ipotee.

Karibu sana katika makala ya leo niliyokuandalia.

Mara nyingi watu wengi wamekuwa wakiogopa kusemwa kwa kuhofia watu watasema nini juu yao.

Neno "watanisemaje" limekuwa chanzo cha wengi kushindwa kupiga hatua na kufikia mafanikio wanayoyataka.

Wengine wameshindwa kuonesha vipaji vyao kwa sababu ya kuogopa kusemwa.

Wengine wameshindwa kuacha tabia mbaya walizokuwa nazo kwa kuogopa marafiki zao watasema nini juu yao.

Wengine wameshindwa kufanya vizuri katika masomo, kazi na mambo mengine mengi kwa kuogopa watu watasema ni ni juu yao.

Leo nataka nikwambia acha uoga uliojijengea juu ya watu. Mafanikio yako yako mikononi mwako, mafanikio yako umeyabeba mwenyewe.

Usigope kusemwa kwani kila unayemuona kafanikiwa amesemwa ila hakuyatilia maanani yaliyosemwa juu yake. Kuna mtu aliyekuwa anawaondoa watu kwenye hofu ya kuogopa kusema aliwaambia "ni kaburini tu ambako watu hawasemwi." Kumbe kama bado unaishi watu watakusema tu.

Jambo jingine watu wanaokusema mara nyingi huwa lengo lao ni kukushusha ili ulingane nao. Hawataki kukuona ukifanikiwa. Ukilijua Ilo  najua utaacha kuogopa kusemwa.

Hata hivyo mti wenye matunda ndiyo utupiwao mawe. Wakikurushia mawe yakusanye yatakusaidia kukujengea msingi. Utakuwa umekomaa na mara nyingi watakusukuma kupambana kuhakikisha kile walichosema hakiwezekani wewe kukifanya kiwezekane.

Kwenye Kitabu Changu kinachoitwa Barabara Ya Mafanikio nimeandika kanuni inayoitwa kanuni ya 20-40-60, usikose nakala yako kujifunza pia kuhusu kusemwa kutoka kwenye kanuni hiyo.

Kumbuka: neno "watanisemaje" limewakosesha wengi mafanikio.

See you at the top

Ni Mimi rafiki na ndugu yako
Edius Bide Katamugora
Author & motivational speaker
0764145476
0625951842 (Whatsapp)
ekatamugora@gmail.com

Karibu sana kuweka oda ya Kitabu changu kizuri kinachofundisha mengi kuhusu mafanikio "Barabara Ya Mafanikio" (The road to success). Nimekuwekea namba zangu hapo juu.

Washirikishe na wenzako kile ulichojifunza.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: