Kuwa na hisia za kutoa
shukrani bila kuzitoa ni kama kuandika barua bila kuituma. Namshukuru Mungu kwa
kuniwezesha leo hii kutimiza miaka kadhaa ya kuzaliwa. Nawashukuru pia wazazi
wangu na nawaombea daima kwa Mungu awazidishie Zaidi na Zaidi. Nawashukuru pia
kwa malezi na elimu bora waliyonipatia. Mungu awabariki.
Aidha namshukuru kila
mmoja aliyechangia kwa namna moja ama nyingine kunifanya leo nimekuwa hivi
nilivyo. Ni kwa neema tu.
Leo mpendwa msomaji ningependa
nikushirikishe mambo 21 muhimu ambayo nimejifunza miaka kadhaa iliyopita.
Mambo hayo, baadhi ni
sehemu ya maisha yangu, mengine nimejifunza kutoka kwenye mazingira niyokulia
na niliyowahi kuishi na ninayoishi, watu niliyokutana nao kwenye maisha yangu,
vitabu nilivyosoma, kutaja machache.
Mambo hayo 21 ni kama
yafuatayo:
1)
Sala na Imani ni vitu muhimu kwenye maisha
ya mwanadamu yeyote. Kila siku kumbuka kumshukuru Mungu na kumuomba Zaidi na
Zaidi. Usiifanye sala kama spea tairi, unapopatwa na matatizo na majanga ndipo
unapokumbuka uwepo wa Mungu. Imani ni kama mswaki,utumie kila siku, lakini
usitumie wa mtu mwingine.
2)
Ipende familia yako na ndiyo iwe mstari wa
mbele kwako. Kama umezaliwa katika familia duni, kubaliana na hiyo hali kama
chagamoto na pambana kuhakikisha familia yako inaendelea.
3)
Ukitumia kipaji chako utafanikiwa kwa
haraka sana kama ukiamua. Kipaji ni kama kito cha thamani machoni pake yeye
aliyenacho, kila kigeukapo ufanikiwa. Kila mtu anapozaliwa anazaliwa na vipaji
na uwezo kuanzia 500-700, cha ajabu kuna wengine bado hawajatambua na kuanza
kutumia vipaji walivyojaliwa. Kuna msemo unasema “Kila mtu amezawadiwa lakini kuna watu hawajawahi kufungua maboksi ya
zawadi zao.”
4)
Kila siku kwako itakuwa kama siku ya
Valentine kama utakuwa kwenye mahusiano na mtu sahihi(everyday will be
Valentine, if you are with the right person.)
5)
Marafiki unaoambatana nao kila siku
watakusaidia ufanikiwe au watakusaidia usifanikiwe. Chagua na ambatana na
marafiki sahihi. Tabia za marafiki zako zinamchango mkubwa kwenye tabia yako. Niambie rafiki yako, nikwambie tabia yako.
6)
Ukiwekeza katika kusoma vitabu na kutafuta
maarifa mbalimbali, utaweza kujiingizia kitabu kwa urahisi sana, kwani ni watu
wachache wanafanya hivyo.
7)
Kuandika kitabu ni alama tosha itakayodumu
vizazi na vizazi.
8)
Unachokijua wewe, kuna watu wengi
hawakijui, hivyo ni vizuri kuwashirikisha ili wajifunze na kufanikiwa. Pia
utaweza kujiingizia kipato kwa kutoa ujuzi ulionao.
9)
Kila unayekutana naye una mengi ya
kujifunza kutoka kwake. Kuwa mwangalifu kila unapokutana na mtu mpya.
10)
Kutoa ni moyo vidole uachia. Ukitoa upendo
na ukarimu kwa watu wote wanaokuzunguka, utapokea upendo na ukarimu kutoka kwa
watu hao pia. Utavuna ulichopanda.
11)
Elimu ya darasani haitoshi ukiishia kusoma
uliyojifunza darasani. Unahitaji kwenda hatua Zaidi na kutafuta maarifa Zaidi.
12)
Elimu yako haipaswi kukutenganisha na
jamii inayokuzunguka, kama ukijitoa kwenye jamii uliyokuwa ukiishi tambua elimu
yako haijakusaidia.
13)
Fursa zipo mahali popote ulipo, huhitaji
kwenda mbali na mahali ulipo kuzitafuta. Mafanikio yapo mikononi mwako. Dig
gold where you are.
14)
Malezi bora ya wazazi yanamchango mkubwa
katika maisha na mafanikio ya watoto wao. Umri mzuri wa kumfundisha mwanao ni
kuanzia pale anapozaliwa hadi anapotimiza miaka 12. Samaki mkunje angali mbichi.
15)
Huhitaji umri mkubwa kufanya mambo makubwa
nay a ajabu. Watu wengi waliofanikiwa walianza wakiwa wadogo.
16)
Mitandao ya kijamii itakusaidia kujulikana
kwa haraka sana na pia kutengeneza branda yako( jinsi unavyojenga picha
vichwani mwa watu pale unapotajwa.) kwa muda mfupi na kwa kutumia gharama ndogo
sana.
17)
Umaskini wa mtu unaanzia kichwani kwake,
sio kukosa mali tu ni mwa kuwa na mtizamo hasi aliyojijengea ndani mwake.
Kumbuka pia pesa ni mtumwa, wewe ni mfalme. Usibadili fomula hiyo kwenye maisha
yako.
18)
Uvumilivu na subira ni kitu muhimu san
hasa kwenye kuanza kuonesha vitu ulivyojaliwa navyo kama kipaji na ujuzi
ulionao n ahata kwenye kufanya biashara. Kumbuka unachokitafuta kinakutafuta
(kanuni ya uvutano), hivyo ni wajibu wako kukitengenezea mazingira sahihi ili
kije kwako. Juhudi, bidii na kujituma view nguzo kuu kwako.
19)
Ukibadilika kila kitu kwenye maisha yako
kitabadilika.
20)
Muda ni kitu muhimu sana kwenye maisha ya
mwanadamu. Ukitambua umuhimu wa muda na kufanya mambo kuendana na muda
utafaikiwa. Habari mbaya ni kwamba muda unapaa, habari nzuri ni kwamba wewe ni
rubani. Kila siku ni muhimu, usikubali ipotee. One day can make you grow.
21)
Ulipozaliwa ulikuja duniani ukilia huku
dunia ikishangilia. Ni wajibu wako mkubwa kubadili kile kilichotokea wakati unazaliwa
pale unapoiaga dunia, yaani unapoiga dunia, wewe unashangilia na dunia
inauzunika kwa sikitiko kuu. Mambo haya yote utayafanya kwa kutimiza kusudi
lako. Anza kwa kujiuliza ulikuja duniani kufanya nini? Kumbuka, Mungu alikuumba
ili uje duniani kutimiza kusudi Fulani. Hakuna aliyezaliwa kwa bahati mbaya.
Hakuna aliyekuja duniani kuzurula na kusindikiza wengine.
Ndimi
EDIUS KATAMUGORA
Author and motivational speaker.
0764145476
0625951842 (Whatsapp)
ekatamugora@gmail.com
washirikishe wenzako ulichojifunza.
kTangazo: Kitabu cha BARABARA YA MAFANIKIO kinaanza kuuzwa rasmi kesho, kwa wale walioweka oda kama unahitaji kitabu hicho karibu kuweka oda kwa mawasiliano hapo juu. Bei ni shilingi 6000, baada ya wiki 2 bei itakuwa 10000.
0 comments:
Post a Comment