Tuesday, 4 July 2017

Tatizo Sio Muda Tatizo Ni Vipaumbele Vyako

Watu wengi wamekuwa wakilalamikia muda na kufikia hatua ya kusema kwamba muda haupo.

Ukweli ni kwamba muda hupo Lakini watu wengi bado hawajatambua matumizi ya muda.

Kila mtu amejaliwa masaa 24 Lakini wale wanaoyatumia vyema na kwa utimilifu ndio tunaowaona wakiwa wamefanikiwa na kubaki midomo wazi. Lakini wanajua muda kwao ni kitu muhimu.

Dangote ana Massa 24, kama wewe, Mohammed Dewj anayo Massa 24 kama wewe. Lakini wao wanafanya zaidi wewe unabaki kulalamika kwamba hakuna muda.

Kwenye kitabu changu cha Barabara Ya Mafanikio nimeandika "Kitu nilichojifunza katika maisha yangu ni kwamba usipochangamkia maisha, maisha yenyewe yatakuchangamkia. Siku zinakimbia na kwa wiki, wiki zinakuwa miezi, miezi inakuwa mwaka, mwaka unakuwa miaka. Usipofanya kitu chochote utabaki mtu mwenye manunguniko na majuto katika maisha yako."

Waingereza wanasema, UA muda ukuue "kill the time and the time will kill you." Muda ni Mali lazima uitumie kama kitu muhimu sana kwenye maisha yako. Muda ni kama shilingi kwenye tundu la choo ikipotea hairudi.

Tatizo LA kupoteza muda linaanzia katika vipaumbele vyetu.

Vipambele ni vile vitu tunavyovichukulia kama vitu vya muhimu sana kwetu.

Jiulize wewe Leo umeweka vipaumbele vyako wapi?;

Je Unatumia muda mwingi kujadili kuhusu Mpira na siasa. Yaani wewe kila siku unajadili kuhusu simba na Yanga. Arsenal na Manchester lakini haujawahi hata kuchukua dakika kumi kujadili kuhusu maisha yako. Unapotea njia.

Unakaa kwenye vijiwe na kuilalamikia serikali kila kukicha. Ndugu yangu kama hujui wewe ni serikali pia. Na hata ikibadilika ndo unatazidi kusema bora ile iliyopita. Anza kufanya mambo yako.

Unapoteza muda kutizama runinga tena vipindi ambavyo havina tija kabisa kwenye maisha yako. Ebu jaribu kufikiri raisi wako angekuwa na yeye kila siku anatizama runinga kwa Masas matano kama wewe. Je nchi ingeenda, nafikiri unajaribu kupata picha. Waziri mkuu naye afanye hivyo hivyo na viongozi wote.

Unapoteza muda ukifuatilia maisha ya wengine, lakini umesahau kufatilia maisha yako mwenyewe. Unajua mtu Fulani analipwa pesa kiasi Fulani tena hupo tayari kubishana mbele ya kadamnasi kuhusu Ilo. Je pesa zake zinakusaidia lolote. Acha kupoteza muda.

Muda wote unatumia mitandao ya kijamii lakini hakuna jipya unalojifunza. Unaweka tu vocha kutajirisha kampuni za simu. Anza kutumia simu yako kutafuta maarifa. Hakuna umaskini kwa mtu anayetafuta maarifa na taarifa sahihi na muhimu. Anza Leo bado haujachelewa.

Weka vipaumbele vyako viwe vitu vyenye tija na vitu vitakavyokusaidia kufanikiwa.

Acha kulalamika kwamba muda haupo. Muda hupo sema umejishikiza kwenye vitu vinavyopoteza muda pasipo wewe kitambua.

Nampenda sana mwandishi ambaye amechangia sana Mimi Leo hii kuwa nilivyo. Dr Fr. Faustin Kamugisha yeye aliwahi kuandika hivi:

"Ukitaka kuujua umuhimu wa mwaka mmoja muulize mwanafunzi aliyerudia darasa. Ukitaka kuujua umuhimu wa mwezi mmoja muulize mama aliyejifungua mwezi mmoja kabla. Ukitaka kuujua umuhimu wa siku mojq muulize mwandishi ambaye anaandika Makala zinazotoka kila siku kwenye gazeti. Ukitaka kuujua umuhimu wa saa moja waulize wapendanao wawili, waliopanga kukutana saa moja lililopita lakini hawakufanikiwa. Ukitaka kuujua umuhimu wa dakika moja muulize msafiri aliyechelewa kupanda ndege."

Utumie muda vizuri. Muda ni Mali. Kila siku uliyonayo ni muhimu. One day can make you grow.

Mafanikio yapo mikononi mwako

Ndimi;
Edius Katamugora (Bide)
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
ekatamugora@gmail.com

Karibu kupata kitabu cha Barabara Ya Mafanikio ambacho kwa Sasa kinapatikana rasmi kwa mawasiliano hapo juu. Tunatuma mikoani pia.

Washirikishe na wenzako ulichojifunza.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: