Jana wakati nipo naandika
Makala zangu nilisikia raisi mstaafu Mh. Jakaya Kikwete akizungumza maneno
ambayo yalinifanya gafla niache kuandika na kusikiliza kwa makini maneno yale aliyokuwa akizungumza. Maneno hayo
yalinivutia kuyasikiliza na hatimaye kupata kitu Fulani ambacho kilimenisukuma
kuandika Makala hii. Mh Kikwete alisema “
Tatizo kubwa la Waafrika wengi ni kulalamika, hata wasomi tunaotegemea watatue
matatizo yetu ndio wamegeuka kuwa walalamikaji wakubwa.”
Huu ni ukweli mtupu
usiopingika, ndiyo maana nimeamua kupigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza
hili ambalo linawapoteza watu wengi. Lakini msumari ninaoupigilia mimi sio wa
kuharibu bali wa kujenga.
Watu wengi wamekuwa
walalamikaji kila kukicha, mara leo hili kesho lile yaani malalamishi hayaishi.
Wasomi wengi ambao tunategemea wamepata maarifa yatakayokuja kujenga jamii zetu
wao ndio wamegeuka kuwa walalamikaji wakubwa.
Ngoja nikwambie ndugu
yangu, malalamishi hayajengi wala hayabadilishi chochote. Acha kulalamika
kabisa maana unapolalamika unaifunga akili yako au ubongo wako ushindwe
kufikiria Zaidi kuhusu suluhisho badala yake unafanya akili yako ikubari kwamba
tatizo Fulani halitatuki. Ukweli ni kwamba kila tatizo lina suluhisho lakini
ukiwa mtu wa kulalamika kila siku huwezi hata siku moja kuona namna ya
kulitatua.
Kumbe jambo la kufanya
leo kama una tabia ya kulalamika kila siku achana nayo, kwanza kabisa hakikisha
tabia hiyo imekufa. Uchunguzi unaonesha kwamba tabia mpya ujengwa ndani ya siku
thelathini yaani mwezi mmoja, kumbe ukilalamika kuhusu jambo Fulani unaweza
kuwa mlalamikaji wa kudumu. Achana na tabia ya kulalamika.
Nakubaliana na Jack Ma
mmiliki na mwanzilishi wa kampuni ya Alibaba raia wa China anayesema “Fursa zimejaa pale watu wanapolalamika.”
Malalamiko ya watu ni fursa tosha. Aliyetengeneza gari alisikia watu
wakilalamika kuhusu umbali mrefu na kuchoka kutembea na farasi na punda. Mwingine
akaona watu wanalalamika kuhusu jua kali, akaamua kutengeneza kofia. Mwingine akaona
watu wanalalamika kuhusu mvua, akaamua kutengeneza mwavuli.
Super Markets zilianza
kama duka tu lakini baada ya watu kulalamika kwanini watu hawawezi kufanya
manunuzi kwa kujichagulia, ndipo watu wakapata wazo la super markets. Kumbe watu
wanapolalamika kumejaa fursa, watu wakilalamika kuhusu uchafu mtaani, ni fursa
kwako kufungua kampuni ya usafi kwenye mtaa wako. Watu wakilalamika, kuhusu
uharifu kwenye mtaa wenu, ni fursa kwako kuanzisha kampuni itakayodumisha
ulinzi mtaani kwenu.
Acha kulalamika, fursa
zimejaa kwenye malalamiko, watu wanapolalamika usiwe mlalamikaji pia. Na wewe
msomi mwenzangu unazingua ujue unapokuwa mmoja wa walalamikaji wakati tunakutegemea
kama suluhisho. Acha kuzingua, acha kulalamika.
"Mafanikio Yapo Mikononi Mwako."
Ndimi
EDIUS KATAMUGORA
AUTHOR AND MOTIVATIONAL SPEAKER
0764145476
0625951842
Email: ekatamugora@gmail.com
Karibu ujipatie kitabu changu cha BARABARA YA MAFANIKIO, Kwa shilingi 6000/= mikoani tunatuma pia.
Imani yangu ni kwamba mafanikio ni kitu cha kushirikishana, washirikishe na wenzio kile ulichojifunza.
0 comments:
Post a Comment