Thursday, 20 July 2017

Maoni Yako Hayapokelewi Kwa Sababu Ya Uwasilishaji

Habari za asubuhi mpendwa msomaji wa Bideism Blog ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na umejiweka tayari kuyatimiza majukumu yako ya Leo.
Tumshukuru Mungu kutupa siku nzuri kama ya Leo.
Leo ni siku muhimu usikubali ipotee hivi hivi. One day can make your grow.

Karibu sana katika makala ya Leo niliyokuandalia.
Unaweza kuwa na maoni mazuri na yenye kujenga na tena yenye tija na watu unaowatolea maoni hayo wakayakataa na kuyapinga kabisa tena wakaacha hata kukusikiliza. Hali kama hii imewahi kunitokea mimi binafsi lakini najua imewahi kukutokea wewe pia katika mazingira Fulani fulani au imewahi kutokea kwa mtu unayemfahamu.

Inaweza kutokea tena katika hali nyingine akaja mtu mwenye maoni duni au yenye tija ndogo, yaani yako ni mazuri zaidi lakini watu wakayaacha maoni uliyotoa wewe wakachukua ya mwenzako tena wakayapokea kwa mikono miwili.

Kwanini hali kama hii inatokea?
Kutopokelewa kwa maoni yako kunasababishwa na namna unavyoyawasilisha. Kwa mfano unaweza kumwambia mtu hivi "Haujapendeza kabisa Leo, jitahidi uwe unavaa vizuri." Mtu huyo anaweza kuyapokea maoni yako au kutoyapokea, lakini ukimwambia hivi "Umependeza lakini ungelivaa hivi ungelipendeza zaidi." Mtu huyo ni rahisi kuyapokea maoni yako.

Leo nakupa siri ambayo ulikuwa huijui au unaijua lakini aujaanza kuitendea kazi au kuitumia. Siri hiyo ni kwamba, watu hawapendi kushurutishwa. Hii ipo hivyo na itabaki kuwa hivyo. Kumbe maoni yetu yanaweza kuwa mazuri na yenye tija lakini ukitoa maoni kwa njia ya kushurutisha maoni yako yana asilimia kidogo ya kupokelewa na kusikilizwa. Watu hawapendi kushurutishwa.

Ukitaka maoni yako yasikilizwe acha kutumia maneno ya shuruti na maoni yako yatapokelewa tena vizuri. Hata wazazi mnapotoa malezi, njia ya kushurutisha sio nzuri. Maneno yenye shuruti ndani yako watoto hawayapokei kirahisi rahisi. Mzazi unapokuwa unamwambia mwanao asome kwa bidii baada ya kushindwa kwenye baadhi ya mitihani, usitumie shuruti katika maoni yako. Usiseme "Acha kucheza sana, ndiyo maana unafeli." Badala yake mwambie "Mwanangu najua wewe ni bora, ukiongeza jitihada na kusoma kwa bidii lazima utafaulu vizuri sana."

Kumbuka maoni yako hayapokelewi kwa sababu unayatoa kwa njia ya kushurutisha.

"Mafanikio Yapo Mikononi Mwako."
Ndimi
EDIUS KATAMUGORA
AUTHOR AND MOTIVATIONAL SPEAKER
0764145476
0625951842
Email: ekatamugora@gmail.com
Karibu ujipatie kitabu changu cha BARABARA YA MAFANIKIO, Kwa shilingi 6000/= mikoani tunatuma pia.
Imani yangu ni kwamba mafanikio ni kitu cha kushirikishana, washirikishe na wenzio kile ulichojifunza.  

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: