Habari za asubuhi mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na umejiweka tayari kutimiza majukumu yako ya Leo. Leo ni siku muhimu usikubali ipotee. One day can make you grow.
Karibu sana katika Makala ya Leo niliyokuandalia.
Kabla ya mwaka 1954 iliaminika dunia nzima kwamba hakuna mtu anayeweza kukimbia maili moja kwa muda wa chini ya dakika nne. Watu wote waliowahi kukimbia mbio walikimbia maili moja kuanzia dakika nne na zaidi, hivyo dunia iliamini dakika nne ndio ukomo au kikwazo cha kukimbia maili moja ambayo ni sawa na kilometa 1.6
Tarehe 6 mwezi mei mwaka 1954 Roger Bannister aliweza kuvuka kikwazo au ukomo huo kwa kukimbia maili moja kwa muda wa dakika 3 na sekunde 59.4 Bwana Roger akawa mtu wa kwanza kuvunja rekodi hiyo ya kikwazo cha dakika nne (The four minute barrier).
Baada ya kitendo hicho kufanywa na Bwana Roger Bannister kilichotokea ni historia. Hadi Leo hii ninapoandika makala hii kuna zaidi ya watu 20000 (elfu ishirini) wameweza kufanya kile alichokifanya Roger Bannister. Ni maajabu yaliyoje.
Mtu ambaye alikuja kuvunja rekodi baadaye ni Landy alivunja rekodi ya Roger Bannister kwa kukimbia maili moja ndani ya dakika 3 na sekunde 43.3 hadi Leo hii rekodi hii haijawahi kuvunjwa.
Tujifunze nini katika hili?
Kwanza kabisa kikwazo cha kwamba kitu Fulani hakiwezekani umekibeba wewe mwenyewe (You are your only limitation).
Hata watu wakikwambia jambo Fulani haliwezekani, wewe sema kwa kuwa ni Mimi litawezekana, wote walioshindwa hawafanani na mimi, mimi sio sawa na wao. Unafikiri Roger Bannister angeweka kikwazo cha dakika nne kichwani angeweza kukimbia dakika 3?, la hasha, yeye alijua ni wa tofauti.
Robert Schuller mchungaji na mwandishi maarufu toka Marekani aliwahi kusema "Ukiniambia jambo Fulani, haliwezekani nitakuuliza lini?." Kumbe kabla ya mwaka 1954 kukimbia kilomita 1.6 chini ya dakika nne jambo hilo lilikuwa haliwezekani lakini mwaka 1954, jambo hilo liliwezekana kupitia Roger Bannister.
Tunakusubiri wewe pia uje kufanya yale mengi ambayo dunia bado inaamini hayawezekani. Kama Roger aliweza, wewe pia unaweza, wote tunayo damu nyekundu hakuna mwenye damu ya kijani wala ya bluu.
"Mafanikio yapo mikononi mwako."
Ndimi:
Edius Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com
Edius Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com
Imani yangu ni kwamba mafanikio ni kitu cha kushirikishana. Mshirikishe na mwenzako makala hii ili naye ajifunze pia.
Jipatie kitabu changu cha Barabara Ya Mafanikio kwa bei ya shilingi 6000/=
0 comments:
Post a Comment