Friday, 25 August 2017

Jinsi Shuhuda Zinavyoweza Kukuza Biashara Yako (How To Use Testimonies To Develop Your Business)

Habari za asubuhi mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na umejiweka tayari kutimiza majukumu yako ya Leo. Tumshukuru Mungu kutujalia siku nzuri kama ya Leo. Leo ni siku muhimu kwenye maisha yako usiruhusu ipotee hivi hivi. One day can make you grow.

Kuonesha umuhimu wa siku moja Mwanamashairi John Burroughs aliwahi kusema "Hii ndiyo siku aliyoifanya Bwana, tuifurahie na tuishangilie."

Karibu sana katika makala ya Leo niliyokuandalia ili uweze kujifunza na kupata maarifa mapya ambayo yatakusaidia kukuinua na kufanikisha malengo yako.

Leo tutajifunza kitu kinachoitwa shuhuda katika biashara. Shuhuda katika biashara naweza kusema ni hile hali ya watu kuonekana wakitumia bidhaa zako au kujitokeza na kusema bidhaa zako zimewasaidia.
Wahenga waliwahi kusema "Kuamini kwa mwafrika, mpaka aone, wengine mpaka waguse ndipo wanapoamini." Makampuni makubwa yamekuwa yakitumia shuhuda kututeka na kutufanya sisi wateja wao. Hapa unakuta wanawachukua watu maarufu na kuwaonesha kwenye matangazo wakitumia bidhaa za kampuni husika.

Makampuni makubwa kama Nike yamekuwa yakiwatumia wachezaji maarufu kama wawakilishi wao na kila wanapokua kwenye michezo mbalimbali wanatumia bidhaa zao. Pepsi wanafanya hivyo pia. Nafikiri umewahi kuona matangazo ya wachezaji wakinywa soda za kopo za Pepsi. Tusiende mbali nafikiri kila siku unamuona Joti anavyozunguka kila kona kwenye TV yako akitangaza matangazo ya Tigo na Dstv.

Kwa kifupi nilichokieleza hapo juu nafikiri umepata maana halisi ya kitu kinachoitwa shuhuda. Imani yangu ni kwamba, kitu chochote kinachofanyika mahali popote duniani unaweza kukihamisha na kukileta kwenye mji au mtaa wako kikaanza kufanya kazi.

Shuhuda nzuri ni za wachungaji;
Hakuna shuhuda nzuri kama za wachungaji na watumishi wa Mungu wanapokua wakisali na kuwaombea watu. Umewahi kuona kwenye TV mtu anakuja na magongo ameyaamsha juu na anasema alikua hawezi kabisa kutembea kwa muda wa miaka 30 lakini sasa hivi anaweza kutembea? Nafikiri umewahi kuona. Ukiona kitu kama hicho Mara 3, akili yako inakusukuma na kuamini kwamba hayo ni ya kweli.

Kama wachungaji wameweza kwanini wewe ushindwe? Hili ndilo swali ambalo unaweza kujiuliza.
Ukweli ni kwamba kama wachungaji wameweza kuzitumia shuhuda kwenye makanisa hivyo basi hata wewe unaweza kutumia shuhuda kukuza biashara zako.

Utawezaje kutumia shuhuda kukuza biashara yako?
Kama unabidhaa unayoiuza mtu yeyote anayekuja kuinunua muombe umchukue picha akiwa anatumia au ameshika bidhaa yako. Baada ya hapo unaweza kuipost picha hiyo katika mitandao ya kijamii inayohusiana na picha kama vile Facebook, Instagram na WhatsApp. Ukiweza kufanya kitu hicho kwa muda mrefu utawavutia wateja wengi.

Ngoja nikwambie siri ambayo ulikua huijui. Watu wengi wanavutiwa sana na picha na pili picha ni kitu rahisi sana kuteka kichwa cha mwanadamu. Kama nilivyotangulia kusema, kuamini kwa mwafrika mpaka aone na kugusa. Watu wengi wapo kama Thomaso, hawaamini mpaka wajionee na kugusa.
                            
                               
                                
( Pichani: Katibu mkuu Wizara Ya Habari, Utamaduni Na Michezo, Profesa Elisante Gabriel, akipokea kitabu changu cha BARABARA YA MAFANIKIO.)

Kuna watu wengi wamekuwa na bidhaa ambazo wanauza lakini wanafanya makosa makubwa kuweka picha ya bidhaa ambayo wanaiuza badala ya kuweka picha pamoja na watumiaji.

Hata kama unauza keki, mtu akija kwako kununua keki mpige picha utuoneshe akiwa na tabasamu anapokua amenunua keki dukani kwako.

Pili picha pia zinajenga mahusiano ya kudumu baina yako na mteja. Mteja akiona umepost picha yake atajua kwamba unamthamini na kumjali hiyo ndiyo Customer care. 

Lakini kumbuka sio kila mtu anapenda kupigwa picha. Kama hata usimlazimishe.

Wachina wanasema "Muda mzuri wa kupanda miti, ulikua miaka ishirini iliyopita. Muda mwingine mzuri ni sasa." Bado haujachelewa anza Leo, anza sasa. Mara tu anapomaliza kusoma makala hii anza kutumia shuhuda.

"Mafanikio yako mikononi mwako."

Ndimi: Edius Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com

Jipatie kitabu cha Barabara Ya Mafanikio kwa shilingi 6000/= tu. Dar es Salaam, Morogoro, Kagera, Iringa, Mwanza tayari vinapayikana. Mikoani tunatuma pia. Mawasiliano; 0764145476/0625951842

Imani yangu mafanikio ni kitu cha kushirikishana. Mshirikishe pia na rafiki, ndugu au jamaa kile ulichojifunza.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

1 comments:

mpeke blog said...

Yah ni kweli kaka. Tunashukuru