Thursday, 24 August 2017

Mwanachuo Fikiria Nje Ya Box

Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na umejiweka tayari kutimiza majukumu yako ya Leo. Tumshukuru Mungu kutujalia siku nzuri kama ya Leo. Leo ni siku muhimu usikubali ipotee. One day can make you grow.
                     
(Piga namba 0764145476 ili kupata kitabu hicho hapo juu)
 
Karibu katika Makala ya Leo niliyokuandalia.

Leo ningependa niandike kitu Fulani kwa wanachuo wenzangu kuwakumbuasha mambo Fulani Fulani ambaye huenda tunayajua au hatuyajui.

Wakati nafikiria na kuitizama elimu yetu ya Tanzania ambayo kila kukicha ibadilisha mambo mengi lakini lengo lake nikutengeneza watu wa kuwaajiri. Toka unasoma darasa LA kwanza hadi sekondari na Leo hupo chuo elimu inatuaandaa kuwa waajiriwa, lakini ajira zenyewe hazipo. Leo hii serikali inawaambia wanavyuo wajiandae kujiajiri lakini hata haijawahi kutoa elimu yoyote ya kujiajiri. Hakuna somo lolote kwenye silabasi inayofundisha kujiajiri.

Wengine watasema kuna elimu kumbakumba (GS) ambayo inafundishwa sekondari na vyuoni kwamba inafundisha kujiajiri lakini ile entrepreneurship unayojifunza imepitwa na wakati.

Sijaandika Makala hii kuilaumu serikali lakini nimeandika makala hii kukimbusha wewe mwanachuo mambo baadhi. Wewe kama mwanachuo unahitaji kufikiri nje ya box. Unahitaji kuacha kufikiri kuajiriwa na huanze kufikiri kujiajiri.

Nayaandika haya kwasababu mambo yamebadilika. Dunia inabadilika na inakimbia kwa kasi ya ajabu sana. Ajira zimekuwa chache. Kama umekuwa mfatiliaji wa Makala zangu nimewahi kuandika kuhusu takwimu za ajira zinazotolewa kila mwaka. Kutokana na sensa ya mwaka 2012, takwimu zinaonesha kwamba, wanahitimu wanafunzi milioni mbili kila mwaka lakini wanaoajiriwa ni laki mbili tu. Umewahi kujiuliza hao milioni moja na laki nane wanakwenda wapi? Ndiyo maana nasema unahitaji kufikiri nje ya box.

Leo hii vyuo vimeongezeka. Kila kukicha vinaanzishwa vyuo vipya. Kile unachokisoma wewe, kuna watu wengi wanakisoma. Degree au diploma yako sio special tena. Ukienda Chuo cha Udom kwa mfano ni kijiji hii inaonesha kwamba watu wengi wanasoma lakini kiwango cha kuajiriwa ni kidogo. The output is not direct proportional to the input.

Jana pia wakati naangalia TV nimekutana na tangazo la benki ya NBC ambalo linaonesha kwamba mtu anaweza kulipia kitu chochote hata kama benki zimefungwa kupitia ATM. Je wale wanaosoma Banking na Finance watakwenda kufanya kazi wapi mifumo kama hii ikianzishwa kwa kila benki? Mwanachuo unahitaji kufikiri nje ya box.

Unatakiwa kufanya nini sasa kama mwanachuo?
 
Kwanza kabisa kitu kikubwa kinachoweza kukufanya kufikiri nje ya ajira ni kufanya biashara. Anza chuoni kwako usisubiri mpaka umalize chuo ndipo uanze kufanya biashara haitakuwa rahisi biashara yako kukua. Ukizingatia ushauri wa Jack Ma bilionea namba moja nchini China na mmiliki wa kampuni ya Alibaba anasema, "Kabla ya miaka 25, inakupasa ufanye uthubutu mkubwa kupita kiasi." Usiseme muda haupo chuoni sijui nabanwa na masomo wakati unapata muda wa kuangalia muvi na series kwako hazipiti mbali, ikitoka tu mpya, mara paap wewe unayo. Bado unasema huna muda? Nakukumbusha tu mmiliki wa Facebook Zuckerberg alianzisha mtandao huo wa kijamii akiwa bado anasoma chuoni. Unahitaji kuanza sasa.

Nakupa siri ya kutafuta kitu utakachouza. Hapa unahitaji kuzingatia mambo matatu:
 
1) Tatuta kitu kinachokosa mfano, nguo
 
2) Tafuta kitu wanachokihitaji (wanapenda kuvaa na kupendeza, ndiyo.)
 
3) Wawe na pesa ya kukilipia (pesa wanazo)
 
Ukizingatia hayo mambo matatu tayari utafanikiwa kwa kiasi kikubwa katika biashara yako.

Pili, anza kutafuta maarifa mbalimbali nje ya kile unachokisoma. Ukiwa na maarifa na taarifa sahihi sio rahisi kukosa kazi ya kufanya. Kwanza watu watakutafuta wenyewe hautakuwa ukijisumbua kuwatafuta au kutafuta ajira. Ninayoyasema Leo nimeyaona na nimeanza kuyafanya na matokeo yake ni makubwa.

Ndimi
Edius Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842
ekatamugora@gmail.com

Kitabu cha Barabara Ya Mafanikio bado kinapatikana. Bei 6000/=

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: