Habari za asubuhi mpendwa msomaji wa BIDEISM BLOG. Ni matumaini yangu kwamba u mzima wa afya na umejiandaa vyema kuianza wiki yako ikiwa Leo ni jumatatu. Tumshukuru Mungu kwa kutujalia kuiona siku njema kama ya Leo kwani wakati wewe unashtuka toka usingizini kuna mwingine alikuwa akipumua pumzi yake ya mwisho. Leo ni siku muhimu sana, usikubali ipotee. One day can make you grow.
Karibu sana katika Makala ya Leo niliyokuandalia.
Miongoni mwa vitu ambavyo siwezi kuacha kabisa kwenye maisha yangu ni kujifunza. Nafikiri uliwahi kusikia watu wakisema "maisha ni mwalimu tosha."
Leo hii nakuandikia Makala hii wewe rafiki yangu mpendwa kukumbusha tu kwani najua umekuwa mtu anayependa kujifunza. Jambo la msingi ambalo litakutofautisha sana na wengine ni maarifa na sio maarifa tu Bali maarifa yanayowekwa katika matumizi. Maana kuna watu wanasoma vitabu kila siku lakini Yale wanayoyapata humo hawayafanyii kazi hivyo maisha yao yanaendelea kuwa yaleyale kila kukicha.
Kitu kikubwa ambacho kitakusaidia kupambana na changamoto za hapa na pale ni kuendelea kujifunza kila siku iitwayo Leo. Unaweza kujifunza kutokana na kusoma vitabu, kusoma makala mbalimbali, kujifunza kipitia watu unaokutana nao kila siku. Jifunze kutokana na mazungumzo unayozungumza na watu Fulani Fulani. Jifunze kutokana na changamoto unazokumbana nazo kila siku. Kumbe siku yoyote tunayopewa na Mungu tumepewa fursa kubwa ya kujifunza hivyo hatuna budi kuitumia fursa hii kwa utimilifu kabisa.
Hakikisha Yale unayojifunza yanakusaidia katika maisha yako, usiyaweke tu kichwani Bali katika matendo, hapo ndipo maarifa yako yatakapo kusaidia. Kama ukiwa mtu wa kujifunza na kutoa kile ulichonacho kuna watu wanaweza kuja na kukulipa pesa kwa sababu msaada au jibu unalo wewe peke yako hivyo hakuna namna lazima wakutafute wewe na kukulipa pesa. Kuna mtu aliwahi kusema "wewe ni maskini kwa sababu hakuna anayejua lolote juu yako."
Kumbe watu wakijua kwamba unayo maarifa Fulani lazima wakutafute na wakulipe na huwezi tena kuendelea kuwa maskini.
Wanasayansi wanasema kwamba pindi ubongo unapojifunza kitu kipya unakuwa na uwezo wa kutengeneza seli mpya. Pili ubongo ni kama misuli, jinsi unavyozidi kuifanyisha mazoezi ndivyo unavyozidi kikomaa. Hata ubongo hupo hivyohivyo ukijifunza unazidi kuuimarisha na kuukomaza. Usiache kujifunza. Kila siku hakikisha kuna kitu ambacho umejifunza.
"Mafanikio yapo mikononi mwako."
Ndimi,
EDIUS KATAMUGORA
AUTHOR AND MOTIVATIONAL SPEAKER
0764145476
0625951842 (WHATSAPP)
Email: ekatamugora@gmail.com
EDIUS KATAMUGORA
AUTHOR AND MOTIVATIONAL SPEAKER
0764145476
0625951842 (WHATSAPP)
Email: ekatamugora@gmail.com
Imani yangu ni kwamba mafanikio ni kitu cha kushirikishana, mshirikishe na rafiki yako kile ulichojifunza.
Usisahau kujipatia nakala ya kitabu changu kizuri cha BARABARA YA MAFANIKIO.
0 comments:
Post a Comment