Habari za asubuhi mpendwa msomaji wa BIDEISM Blog. Ni matumaini yangu kwamba u mzima wa Afya na umeamka salama kutimiza majukumu yako ya Leo.
Leo ni siku muhimu usikubali ipotee.
One day can make you grow.
Leo ni siku muhimu usikubali ipotee.
One day can make you grow.
Karibu sana kusoma kile nilichokuandalia Leo hii.
Mara nyingi nimekuwa nikitafuta mambo yanayowafanya wanavyuo wengi kushindwa kutimiza ndoto na malengo yao. Ndiyo maana nikaamua kuandika taa 8 nyekundu zinazowamulika wanavyuo na wahitimu wa vyuo.
Leo hii kumekuwa na ukosefu wa ajira lakini sababu kubwa ni zile nitakazozitaja hapa. Taa nyekundu Mara nyingi huonesha alama ya simama(stop) kumbe hata wanavyuo na wahitimu wa vyuo kuna taa 8 zinazowamulika ambazo mnatakiwa kuzifahamu na kuzibadili ziwe za kijani.
Taa 8 nyekundu ni kama zifuatazo;
1. Umaskini wa mawazo (poverty of ideas and ideology of poverty);
Wapo wanavyuo wengi ambao ukiwauliza unawezaje kutumia ujuzi wako wa darasani kujiajiri? Watakwambia kwamba hawawezi. Hii hipo wazi Leo hii kuna wanafunzi wengi wanasoma mambo ya biashara lakini ukiwaambia hata wakupe wazo moja la biashara hawana.

2. Kuwa walalamikaji kila kukicha (excuses oriented):
Wanavyuo wengi wamekuwa wakiilalamikia serikali kwamba haitoi ajira za kutosha lakini wamesahau kwamba kila mwaka wanahitimu wanavyuo milioni 1.2, hii inapelekea serikali kuajiri wahitimu laki 2 tu kwa mwaka kadri ya sensa ya mwaka 2012. Mwanachuo anza sasa kujipanga ni kwa namna gani utaweza kujiajiri, weka wazo kichwani kwamba unatakiwa kujitegemea sio kuitegemea serikali. Saikolojia inasema "mtu anapoweka kitu kichwani, anaweza kukifanya kiwe cha ukweli."

3. Kuhitaji mishahara minono zaidi ya kazi wanazozifanya. (High pay oriented than output);
Wengi wa wasomi hufikiri kwamba wanapohitimu vyuo wanatakiwa kufanya kazi zinazowalipa kipato kikubwa. Kazi zinazolipa mishahara midogo wanazidharau lakini bado wanazunguka na barua za kaki.
Wengi wa wasomi hufikiri kwamba wanapohitimu vyuo wanatakiwa kufanya kazi zinazowalipa kipato kikubwa. Kazi zinazolipa mishahara midogo wanazidharau lakini bado wanazunguka na barua za kaki.
4. Akili Tegemezi (High dependency syndrome):
Wasomi wengi wanategemea kupata kila kitu kutoka kwa mwalimu (spoon feeding). Hakuna mwalimu yoyote duniani atakayekuja kukufundisha kila kitu ikiwa wewe huwezi kujiongeza kutafuta maarifa zaidi.
Wasomi wengi wanategemea kupata kila kitu kutoka kwa mwalimu (spoon feeding). Hakuna mwalimu yoyote duniani atakayekuja kukufundisha kila kitu ikiwa wewe huwezi kujiongeza kutafuta maarifa zaidi.
5. Umaskini Wa Akili za Kibunifu:
Hapa kuna aina tatu za akili. 1) Akili za kawaida: Watu wenye akili za kawaida hushangaa kile wengine wanachofanya (many wonder)
(2) Akili za katikati (average mind): hawa huona tu vitu vinafanyika ( They look at things happening)
(3). Akili Kubwa : hawa ndio wafanyaji, kama wamesomea kitu, wanakiweka katika matumizi. Mtu kama amesoma mambo ya biashara anao uwezo wa kuanzisha biashara na ikakua. Kama amesomea udakatari ana uwezo wa kuanzisha hospitali yake kutaja wachache.

6. Wasomi wengi wanauza vyeti zaidi ya ujuzi; siku hizi waajiri hawaangalii vyeti vyako, kitu cha kwanza kuangalia ni ujuzi wako. Tafuta kwanza ujuzi lakini kumbuka vyeti pia ni kigezo. Tanguliza ujuzi ndipo vyeti vyako vifuate.
7. Utumwa wa mtandao (Digital slavery): wasomi wengi wametekwa sana na mitandao ya kijamii. Ni watumiaji wazuri wa WhatsApp, Facebook na Instagram. Hakikisha wewe sio mtumwa wa mtandao. Tumia intaneti kujifunza mambo yatakayo kusaidia. Uzuri wa intaneti Ina kila kitu unachoweza kujifunza. Kumbuka pia huu ni ulimwengu wa taarifa. Tafuta taarifa sahihi zitakazo kusaidia. "Manage ICT don't let ICT manage you."
8. Mbinu mbovu za kuingia kwenye soko la ajira: kuna wimbi kubwa la wasomi hawajui kuandika CV zao vizuri. Wengine hawana ujuzi wowote unaohusu usaili (interview). Anza Leo kujifunza namna ya kuwasiliana na watu. Njia nzuri ya kujifunza ni kujitokeza pale mnapopewa kazi ya kuwafundisha wengine( presentation). Hakikisha kwenye presentation inahusika ipasavyo, hapo utaweza kuhumudu usaili kwani presentation zinajenga ujasiri. Anza pia kujifunza kuandika CV hata kama wewe ni mwaka wa kwanza.
Mafanikio yapo mikononi mwako."
Ndimi,
EDIUS KATAMUGORA
AUTHOR AND MOTIVATIONAL SPEAKER
0764145476
0625951842 (WHATSAPP)
Email: ekatamugora@gmail.com
Imani yangu ni kwamba mafanikio ni kitu cha kushirikishana, mshirikishe na rafiki yako kile ulichojifunza.
Usisahau kujipatia nakala ya kitabu changu kizuri cha BARABARA YA MAFANIKIO.
2 comments:
Ujumbe mzuri. Asante mkuu tutafanyia kazi
Good sana, na appreciate bro
Post a Comment