Jana dunia nzima ilitikiswa na habari ya kuhama kwa mchezaji machachali Neymar Santos Jr kutoka Barcelona kwenda timu ya Paris Saint-German (PSG).
Ununuzi wa Neymar haukuishia hapo tu bali umemfanya kuwa mchezaji ghari duniani na pia mchezaji anayelipwa pesa nyingi kuliko wote duniani. Neymar amenunuliwa kwa Yuro zisizopungua milioni 200 huku akilipwa Yuro 3.065 kwa saa, Yuro 73571 kwa siku, Yuro 515,000 kwa juma, Yuro 2,060,000 kwa mwezi na Yuro 24,720,000 kwa mwaka.
Rafiki yangu Christopher Chaula ambaye ni mpenzi wa timu ya Barcelona alinitumia ujumbe huu "Iwapo unaweza kujiwekea Tsh 2,239,300 kwa siku, kila siku unaweza kumnunua Neymar baada ya miaka 718."
Usiyoyajua kuhusu Neymar:
Alizaliwa tarehe 5, februari mwaka 1992 huko Mogi das Cruzes nchini Brazil. Hivyo ana miaka 25 hadi sasa.
Aliwahi kuzichezea timu za Portugues Santista (1999-2003), Santos (2003-2009), timu ya watoto, Santos (2009-2013), timu ya wakubwa, Barcelona (2013-2017) na sasa ni mchezaji wa PSG ya Ufaransa toka jana tarehe 4/8/2017 lakini pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Brazil.
Katika timu yake mpya ya PSG atacheza kama mshambuliaji akivalia jezi namba 10.
Nilichojifunza kutoka kwa Neymar;
Kwanza kabisa kipaji ni kitu cha kipekee kinachoweza kukuletea mafanikio kwa muda mfupi sana. Neymar umaarufu wake umeanza mwaka 2013 alipokuwa akipewa sifa kedekede na Pele ambaye mchezaji wa zamani wa Brazil macho ya dunia nzima yakaelekezwa kwake. Ndipo timu ya Barcelona ikaamua kumnunua mwaka huo huo. Kwenye kitabu changu cha Barabara Ya Mafanikio nimeandika "uchunguzi unaonesha kwamba, kila binadamu anapozaliwa, anazaliwa akiwa na uwezo na vipaji kuanzia 500-700, lakini watu wengi hawatumii kipaji hata kimoja."
Ndiyo maana kuna mtu aliwahi kusema "Kila mtu amezawadiwa lakini kuna watu hawajawahi kufungua maboksi ya zawadi zao." Usikubali kufa na kipaji chako kama Dr Myles anavyosema kwamba "Makaburini ndiyo sehemu tajiri kuliko sehemu zote dunia. Watu wamekufa na vitabu bila kuviandika, nyimbo bila kuziimba, viwanda bila kuvigundua, vipaji lukuki bila kuvitumia, kutaja wachache." Anza Leo kutumia na kuonesha kipaji chako.
Kujituma;
Neymar ni mchezaji anayejituma sana akiwa uwanjani, madoido na chenga zake hazijawahi kumuacha mtu salama. Aliwahi kumpiga mchezaji mmoja chenga hadi akafariki papo hapo, kwenye kaburi la mchezaji hiyo yameandikwa maneno "killed by Neymar Santos Jr." Yaani "Aliuliwa na Neymar Santos Jr."
Ushirikiano:
Neymar amekuwa akishirikiana na wenzake vizuri sana uwanjani, kuanzia timu yake ya taifa hadi kwenye timu yake aliyotoka ya Barcelona huku akiwa mshirika nzuri wa kina Messi na Suarez.
Kumbe haya mambo matatu ni muhimu sana kwenye maisha yetu na ya kujifunza siku ya Leo. Ukiwa na kipaji usiishie tu kuwa nacho, unalala na kuamka, hakikisha watu wanaokuzunguka wanatambua kipaji chako, jitume kadri uwezavyo kuhakikisha wewe ni bora katika matumizi ya kipaji chako, kila siku Fanya kitu kinachohusiana na kipaji chako. Kumbuka pia kushirikiana na wenzako maana "Ukitaka kwenda haraka tembea peke yako, ukitaka kwenda mbali tembea na wenzako." Ni methali ya watu wa Kenya.
Anza Leo kutumia kipaji chako, usibweteke. Kuna kitu kikubwa nakiona ndani yako kama ukikubali na kuanza kutumia kipaji chako. Usibweteke. Amka sasa wakati wako ndio Leo, wakati wako ndio sasa.
"Mafanikio yapo mikononi mwako."
Ndimi,
EDIUS KATAMUGORA
AUTHOR AND MOTIVATIONAL SPEAKER
0764145476
0625951842 (WHATSAPP)
Email: ekatamugora@gmail.com
Imani yangu ni kwamba mafanikio ni kitu cha kushirikishana, mshirikishe na rafiki yako kile ulichojifunza.
Usisahau kujipatia nakala ya kitabu changu kizuri cha BARABARA YA MAFANIKIO.
0 comments:
Post a Comment