Habari za asubuhi mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka mapema na umejiweka tayari kutimiza majukumu yako ya Leo. Tumshukuru Mungu kwa kutujalia siku nzuri kama ya Leo. Leo ni siku muhimu sana kwenye maisha yako usikubali ipotee hivi hivi. One day can make you grow.
Hakuna kitu chenye thamani sana kama muda. Ndiyo maana kuna watu waliwahi kusema "Poteza muda, ukupoteze pia." Muda ni kitu muhimu sana kwenye maisha yetu. Muda ni Mali. Muda ni aseti.
Watu wengi wamekuwa na majukumu mengi ambayo wameshindwa kuyatimiza na hatimaye kuyaweka viporo na mwisho wa siku hawayafanyii kazi kabisa.
Rafiki yangu muda ukienda haurudi. "Habari mbaya ni kwamba muda unapaa. Habari nzuri ni kwamba, wewe ni rubani." Anasema Michael Alshuler. Kuhusu muda pia Carl Pandburg alikuwa na haya ya kusema "Muda ni shilingi ya thamani sana katika maisha yako. Wewe na wewe peke yako ndiye utakayeamua jinsi gani utaweza kuitumia. Kuwa mwangalifu watu wengine wasije wakaitumia kwa ajili yako."
Utawezaje kutimiza majukumu yako kila siku?:
Watu wengi wanajiwekea malengo mengi ya kutimiza kila siku lakini hadi siku inafikia ukomo wanakuwa wamefanikiwa kutimiza majukumu machache lakini mengine hawayatimizi.
Watu wengi wanajiwekea malengo mengi ya kutimiza kila siku lakini hadi siku inafikia ukomo wanakuwa wamefanikiwa kutimiza majukumu machache lakini mengine hawayatimizi.
Hali kama hiyo hujitokeza kwa namna mtu anavyopangilia muda wake. Jinsi unavyopangilia muda wako ndivyo unavyojiruhusu kutimiza majukumu yako ya kila siku.
Ifahamu Sheria Ya Parkinson
Cyril Northcote Parkinson alizaliwa tarehe 30 July 1909 huko Bernard Castle katika nchi ya Uingereza. Amekuwa askari Maji na amekuwa mwandishi wa vitabu zaidi ya 60. Aliaga dunia tarehe 9, mwezi Machi, mwaka 1993 akiwa na miaka 83.
Cyril Northcote Parkinson alizaliwa tarehe 30 July 1909 huko Bernard Castle katika nchi ya Uingereza. Amekuwa askari Maji na amekuwa mwandishi wa vitabu zaidi ya 60. Aliaga dunia tarehe 9, mwezi Machi, mwaka 1993 akiwa na miaka 83.
Mwaka 1957 aliweka sheria yake aliyoiita jina lake (Parkinson's Law). Sheria hii inasema "Kazi huongezeka kufuatana na muda wake wa kuikamilisha." Au "Kazi hufanyika kutokana na muda uliopo au muda maalumu."
Kumbe ili uweze kutimiza majukumu yako unahitaji kupanga majukumu yako katika muda maalumu yaani katika masaa. Mfano kama ni mwanafunzi sema hivi "Nitasoma somo Fulani kuanzia saa3 asubuhi hadi SAA 5." Lakini usiseme hivi "Nitasoma usiku." Kumbuka usiku unaanzia saa1 hadi saa6 usiku kumbe akili yako inaanza kukushawishi na kukwambia utasoma baadae mwisho wa siku utakuta haujatimiza kile ulichokipanga kukifanya.
Uzuri wa Sheria hii ya Parkinson ni kwamba inaruhusu akili na ubongo wako kukimbizana na muda na utajikuta umetimiza malengo na majukumu yako kila siku. Usiseme nitafanya kitu Fulani asubuhi au mchana au jioni, sema nitafanya kazi Fulani kuanzia saa fulani hadi Fulani. Hakikisha unaifata sheria hii ya Parkinson itakusaidia sana kutimiza kazi zako za kila siku na utaona unao muda wa ziada.
Tatizo la kuona muda hautoshi linaanzia pale tunapokwenda kinyume na Sheria hii ya Parkinson. Furaha yangu ni kukufundisha kitu kitakachokusaidia kwenye maisha yako. Anza mara moja kutumia kanuni hii utaona mabadiliko makubwa na utaweza kufanya kazi zako zote kama ulivyozipanga na kuzikamilisha.
Nakutakia utekelezaji mwema rafiki yangu.
"Mafanikio yako mikononi mwako."
Ndimi:
Edius Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com
Edius Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com
Jipatie
kitabu cha Barabara Ya Mafanikio kwa shilingi 6000/= tu. Dar es Salaam,
Morogoro, Kagera, Iringa, Mwanza tayari vinapayikana. Mikoani tunatuma
pia. Mawasiliano; 0764145476/0625951842
Imani yangu mafanikio ni kitu cha kushirikishana. Mshirikishe pia na rafiki, ndugu au jamaa kile ulichojifunza.
0 comments:
Post a Comment