Siku yangu ya kwanza kufika mahali ninapofanyia kazi nilipigwa na butwaa na tahamaki ya hali ya juu sana.
Hali hii ilinitokea pale nilipomuona dada mmoja akiendesha magari ya kutengeneza Barabara. Kusema kweli kila wakati nilipomuona huyo mdada sikuchoka kumtizama na kuona jinsi anavyopiga kazi.
Nilipokuwa kidato cha kwanza nilisoma kitabu cha Hawa the Bus Driver ambacho Mimi nilijua ni hadithi tu kwani toka nizaliwe sikuwahi kuona mwanamke akiendesha magari makubwa kama malori, mabasi na magari ya kutengeneza Barabara.
Siku chache baadaye nilitengeneza urafiki na dada Sofia shauku yangu ilikuwa nijue kuendesha vyombo kama vile akijifunzia wapi. Kwa maana moja ya tabia ambayo ninayo hadi Leo hii ni kutaka kujifunza toka kwa mtu yeyote nikiona kuna kitu naweza kujifunza kutoka kwake. Hii ni tabia ambayo hadi Leo hii imenifanya nijue mambo mengi.
Basi bwana, siku yangu ya kumuuliza maswali Dada Sofia ikafika nikasema ngoja nimuulize alijifunzia wapi kuendesha magari mazito na makubwa kama yale wakati pale kazini kuna wanaume wengi ambao kazi zao ni kubeba zege na wengine hata kuokota mizizi wakati wa kusambaza vifusi!. Dada Sofia aliniambia kwamba "Mimi sijaenda shule, vitu vyote nimejifunza hapa kazini. Wakati wanatengeneza barabara ya Iringa-Makambako ndipo nilipojifunza kuendesha magari haya. Hapo aliniacha mdomo wazi.
Akili yangu mimi ilinituma labda alikwenda kusomea kozi Fulani Veta ndipo akapata hile kazi la hasha! Yeye kujifunza kila kitu kazini.
Tujifunze nini kutoka kwa dada huyu?:
1) Tusibague kazi
Mimi na wewe tunafikiri labda kuendesha magari ya kutengeneza Barabara (Motor graders, excavators) ni kazi za wanaume lakini Sofia ametuonesha kwamba hatupo sahihi. Pia watu wengi hasa wasomi wamekuwa wana tatizo kubwa la kubagua kazi kisa eti aiendani na kitu walichokisoma. Ukiendelea na tabia hiyo ndugu yangu hiyo bahasha yako ya kaki itakuwa inachanika tu, unanunua nyingine lakini vyeti vyako havipokelewi. Badilikeni.

2) Unaweza Kujifunza Kila Kitu Kama Ukithubutu;
Dada Sofia ni moja kati ya watu wenye nguvu kubwa ya uthubutu. Alisema najifunza na akajifunza. Leo hii kuna watu wapo maeneo Fulani ya kazi miaka nenda rudi hawajifunzi kitu kipya. Sehemu walizopo zinakazi nyingi ambazo mtu anaweza kujifunza lakini wenyewe hawajifunzi wanaishia tu kudai mishahara iongezeke. Ndugu yangu na wewe kama hupo kwenye kundi hili toka haraka anza kujifunza. Wewe sio mtu wa kubeba zege miaka mitano anza na wewe kujifunza ujenzi. Ukiweza kujifunza ama kwa hakika utanipenda.

3) Kujituma:
Moja kati ya watu wanafanya kazi kwa bidii ni dada Sofia. Yeye ni mtu anayependa sana kujituma. Ngoja nikwambie kitu rafiki yangu bidii haijawahi kumuangusha mtu hata siku moja. Wahenga walisema "mchumia juani, hulia kivulini." Hata maandiko yanasema "Mtu mvivu hushindwa hata kupeleka mkono wa chakula mdomoni."

4) Usidharau Kazi Ya Mtu:
Hiki ni kitu ambacho hapo juu sijakigusia kabisa lakini dada Sofia aliniambia kwa kazi yake ameweza kununua kiwanja na kujenga nyumba kubwa tu kwa kupitia kazi yake. Wale wadada mnaotegemea wanaume kuwafanyia kila kitu, Sofia awe mfano wa kuigwa. Vya bure vina gharama.

Siku moja aliniambia waliwahi kuja wanafunzi kutoka Veta kuomba kazi ya kuendesha magari ya kutengeneza Barabara. Yeye alipewa kazi ya kuwapitisha kama wanaweza au la. Kadri ya yeye anadai walichokuwa wanajua ni majina ya sehemu za magari yale lakini walikuwa hajafahamu vizuri kuendesha magari yale. Dada Sofia alijitolea kuwafundisha kila siku kuanzia sa 11 alfajiri ilihali bosi asijue hadi wale vijana waliweza kuendesha magari yale na baadae walipata kazi ya kupakia vifusi kwenye maroli na kazi zinginezo. Usimdharau usiyemjua.
Imani yangu na wewe umejifunza mengi kupitia dada Sofia.
"Mafanikio yako mikononi mwako."
Ndimi:
Edius Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com
Edius Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com
Jipatie
kitabu cha Barabara Ya Mafanikio kwa shilingi 6000/= tu. Dar es Salaam,
Morogoro, Kagera, Iringa, Mwanza tayari vinapayikana. Mikoani tunatuma
pia. Mawasiliano; 0764145476/0625951842
Imani yangu mafanikio ni kitu cha kushirikishana. Mshirikishe pia na rafiki, ndugu au jamaa kile ulichojifunza.
0 comments:
Post a Comment