Saturday, 26 August 2017

Sio Kila Unaloambiwa Ni La Kweli

Habari za asubuhi mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na umejiweka tayari kutimiza majukumu yako ya Leo.
Leo ni siku muhimu usikubari ipotee hivihivi. One day can make you grow.

Karibu sana katika makala ya Leo niliyokuandalia.

Mara nyingi tumekua tukipokea maoni na ushauri kutoka kwa watu mbalimbali. Maoni mengi yamelenga kutubadilisha na kutuendeleza sisi. Lakini sio kila unaloambiwa ni la kulichukua jinsi lilivyo na kulifanyia kazi.

Watu wengi wanaweza kukupotosha kama ukifuata kila kitu wanachokwambia. Ipo wazi mtu anapotoa maoni yake Mara nyingi hutoa maoni yake kutokana na yeye anavyokichukulia kitu. Hivyo unahitaji maskio yenye chujio litakalo kusaidia kujua ni lipi la kufanyia kazi na ni lipi la kuacha.

Watu wengi wamepoteza ndoto zao kutokana na kile walichoambiwa na ndugu, jamaa au marafiki. Kuna watu walikuwa na ndoto kubwa na pia malengo makubwa lakini maneno walioambiwa na watu yaliwavuruga na kuacha kile walichotaka kukifanya.

Mtu wa mfano aliyekataa kile alichojua anakifanya ni Yosefu. Yeye ndugu zake walimwambia huwezi kuwa kiongozi wetu na hatimaye wakamuuza kwenye nchi ya utumwa Misri, lakini kwake haikua kikwazo. Aliishia kuwa waziri mkuu wa Misri na hatimaye kuwasaidia ndugu zake pamoja na baba yake walipokuwa na balaa la njaa. 

.Kuna watu wengi ambao kama wangechukua kile walichoambiwa na watu wengine dunia hii ya Leo isingewatambua. Lakini kutokana na kuwa na akili pembuzi ya kile walichoambiwa Leo hii wanafahamika duniani kote, hawa ni kama wafauatao:

Thomas Edson;
Huyu ndiye aliyegundua umeme kupitia taa inayowaka na mwanzilishi wa kampuni inayoitwa General Electric Corporation. Akiwa katika madarasa ya chini kabisa ambapo tunaweza kusema kama shule ya msingi mwalimu wake alimwandikia ujumbe uliosomeka "Mwanao ni mpumbavu, hawezi kujifunza, mwondoe shuleni." Mama yake baada ya kuusoma ujumbe hule alijibu "Mtoto wangu ni mpumbavu na hawezi kujifunza. Nitamfundisha mwenyewe." Nafikiri isingelikuwa mtazamo chanya wa mama yake hadi Leo hii tungelikua tunatumia vibatari, taa za chemli na mishumaa. Edson pia ndiye mgunduzi wa kamera.

Oprah Winfrey:
Huyu ni mwanamama mashuhuri duniani ambaye amekua akiandaa vipindi vya televisheni vinavyotizamwa kila kona ya dunia na amekuwa akiwahoji watu maarufu. Siku ya kwanza anaenda kuomba kufanya shughuli ya utayarishaji wa vipindi vya TV katika usaili, aliambiwa yakwamba hawezi lolote na hana sura nzuri ya kuonekana kwenye TV. Baada ya hapo kilichotokea ni historia. Oprah ni maarufu Leo kupita kiasi na amekuwa kati ya wanawake matajiri duniani. Unafikiri angechukua maneno akiyopewa angeweza kufika hapo! Hapana. Sio kila unaloambiwa ni la kuchukua.

Beyonce;
Anafahamika kama mwimbaji maarufu wa kike duniani kutoka nchini Marekani. Siku ya kwanza wakati anafanya usaili wa kuingia kwenye mashindano ya kuimba aliambiwa kwamba, hana sauti nzuri ya kuimba na hawezi kuimba. Leo hii ndiye huyu huyu anayeimba kwa sauti nzuri na dunia nzima inamtambua.

Watu wakikwambia maneno au ushauri Fulani. Unahitaji kuchukua ushauri mzuri na kuacha hule unaaona haukufahi. Tumia akili pembuzi kwa kila ushauri unaopewa. Chekecha maneno ya watu. Husiruhusu watu wakupangie maisha yako kama kweli unajua unachokifanya.

"Mafanikio yako mikononi mwako."

Ndimi: Edius Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com

Jipatie kitabu cha Barabara Ya Mafanikio kwa shilingi 6000/= tu. Dar es Salaam, Morogoro, Kagera, Iringa, Mwanza tayari vinapayikana. Mikoani tunatuma pia. Mawasiliano; 0764145476/0625951842

Imani yangu mafanikio ni kitu cha kushirikishana. Mshirikishe pia na rafiki, ndugu au jamaa kile ulichojifunza

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

1 comments:

Unknown said...

Na barikiwa sana nakuona asubuh yangu itafika