Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na umejiweka tayari kutimiza majukumu yako ya siku ya Leo.
Tumshukuru Mungu kutujalia siku nzuri kama ya Leo. Leo ni siku muhimu usikubali ipotee. One day can make you grow ( siku moja inaweza kukufanya ukue.)
Tumshukuru Mungu kutujalia siku nzuri kama ya Leo. Leo ni siku muhimu usikubali ipotee. One day can make you grow ( siku moja inaweza kukufanya ukue.)
Karibu sana katika Makala niliyokuandalia siku ya Leo.
Kama umefanikiwa kusoma kitabu changu cha Barabara Ya Mafanikio katika sura ya pili niliyoiita "Ili Ufanikiwe Lazima Uamke Muda Huu." Nimeeleza yakwamba muda mzuri wa kuamka kwa watu wengi waliofanikiwa ni sa 11 alfajiri. Kama haujafanikiwa kusoma kusoma kitabu hicho umefanya makosa makubwa kama wewe ni mwanamafanikio. Lakini yote kwa yote bado haujachelewa, nakala bado zipo zinauzwa.
Wengine wakiona saa 11 alfajiri watakwambia ni mapema mno lakini watu wengi waliofanikiwa wanaamka muda huo, na wamekuwa wakifanya hivyo kila siku. Kuamka mapema kutakusaidia mambo yafuatayo;
1) kupata muda wa kutafakari na kusali kumuomba Mungu.
2) Hakuna mengi ya kutizama katika mitandao. Ukizingatia siku hizi watu wanaamka na kushika simu zao na kuingia kwenye mitandao ya kijamii kumbe ni makosa makubwa.
3) Kupata muda wa kufanya mazoezi ya mwili. Kumbuka mazoezi yanasaidia kujenga mwili na kutunza afya pia.
4) Kwa wanafunzi, muda huu ni mzuri sana kwenye kusoma kwa ubongo wako unakuwa na tabia ya sponji yaani unaweza kufyonza mambo mengi, hii ni kutokana na uchunguzi uliofanywa na wataalamu kutokana chuo kikuu cha California, Berkeley walioongozwa na Dkt. Mathew Walker.
5) Hakuna usumbufu. Kama wa watoto, kelele za miziki na kadhalika. Hivyo unafanya mambo yako kwa utulivu.
(6) Unapata muda wa ziada. Saa kumi na moja alfajiri kitaalamu inaitwa Time for legends. Unaweza kufanya mambo mengi hadi kufikia asubuhi ambapo wengi wanakua wamelala. Kumbuka kila siku ukiamka jua limechomoza, unafanya makosa makubwa. Jifunze kuamka mapema.
(7) Ukiamka mapema utaweza kusoma Vitabu vingi na kuweza kukuza fikra zako. Ikumbukwe "Hakuna umaskini kwa mtu anayeendeleza na kukuza fikra zake." Kumekuwa na watu wengi wananiambia wanashindwa kusoma Vitabu, lakini ukijenga mazoea ya kuamka mapema muda wa kusoma Vitabu hauwezi kukosa.
Yote niliyoyaandika hapo juu, yameelezwa kwenye kitabu changu cha Barabara Ya Mafanikio.
Tatizo liko wapi?.
Kuamka mapema ni tabia kama zilivyo tabia nyingine. Hivyo unapaswa kuijenga. Uchunguzi unaonesha kwamba tabia mpya uweza kuwekwa katika vitendo ndani ya siku 30 ambayo ni takribani mwezi mmoja. Kumbe ili ufaulu kuamka saa11, lazima upitie maumivu makali ya kufanya mazoezi ya kuamka muda huo.
Kama nilivyotangulia kusema, tabia mpya hujengwa ndani ya siku 30, hivyo ukifanikiwa kuamka saa11 ndani ya siku 30, utaweza kumudu kuamka muda huo maisha yako yote na hii itakusaidia sana.
Kuna mtu ataanza kuamka mapema lakini baada ya wiki anaacha.
Kuna mtu ataanza kuamka mapema lakini baada ya wiki anaacha.
Jinsi ya kuweza kuamka mapema;
Waandishi wa kitabu cha The Miracle Morning For Writers, Hal Elrod na Steve Scott wametoa njia nzuri ambazo ukizitumia unaweza kufaulu kuamka mapema kila siku. Hizi njia ni tano ambazo ni kama zifuatazo;

1) Weka malengo kabla ya kulala;
Kabla haujalala weka malengo kwamba kesho nikiamka nitafanya mambo kadhaa. Mfano kama ni mwandishi, kesho nitaandika kuhusu vitu kadhaa.
Kabla haujalala weka malengo kwamba kesho nikiamka nitafanya mambo kadhaa. Mfano kama ni mwandishi, kesho nitaandika kuhusu vitu kadhaa.
2) Weka alamu mbali na kitanda chako;
Watu wengi wamekuwa wakiweka alamu lakini zinapolia wanaamka haraka na kuzizima wakati wameziweka wenyewe. Sio wewe tu hata mimi nilikua nikifanya hivyo lakini nimeacha. Ili huweze kuepuka jambo hilo hakikisha alamu ambayo umeiseti hipo mbali na kitanda chako kiasi kwamba inakubidi uamke na kutembea ili uizime. Ukifanikiwa kufanya hivyo sio rahisi tena kwako kurudi kitandani.

3) Fanya usafi wa kinywa:
Mara tu baada ya kuzima alamu, nenda kafanye usafi wa kinywa chako.
Mara tu baada ya kuzima alamu, nenda kafanye usafi wa kinywa chako.
4) Kunywa Glasi ya maji:
Baada ya kufanya usafi wa kinywa tayari utakuwa umekuwa msafi kinywani hivyo unashauriwa kunywa glasi moja ya maji au zaidi. Umesikia maji ni uhai. Ukinywa maji Mara tu baada ya kuamka unafanya mwili wako uwe mchangamfu siku nzima. Usisubiri mpaka uandikiwe dozi na daktari ndo ukumbuke kunywa maji. Fanya kunywa maji kwako kama tabia. Lakini pia kama umefatilia watu wengi wanaokunywa maji sana hawaugui hovyohovyo. Wataalamu wanasema kila mwanadamu inabidi anywe Lita moja na nusu ya maji kwa siku kwa kiwango cha chini. Ili unywe maji yako vizuri asubuhi yaandae kabla ya kulala.

5) Vaa nguo zako za mazoezi au ingia bafuni uoge;
Unaweza kuanza kufanya mazoezi au kama haujisikii kufanya mazoezi ingia bafuni ujimwagie maji. Hii itakufanya uamke kabisa na usahau kabisa kuhusu usingizi. Nimekumbuka tukiwa jeshini ukionekana unalala unamwagiwa maji, lazima uamke tu na usingizi ukate hapo hapo hata kama una usingizi mzito namna gani.

Ukitekeleza mambo niliyoyataja hapo juu, utajiweka katika wakati mzuri wa kuamka mapema na kutimiza ndoto zako.
"Mafanikio yapo mikononi mwako."
Ndimi:
Edius Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com
Imani yangu ni kwamba, Mafanikio ni kitu cha kushirikishana.
Mshirikishe na rafiki yako ili naye apate kujifunza.
Kitabu cha Barabara Ya Mafanikio bado kinapatikana kwa shilingi 6000/= tu. Dar, Morogoro, Iringa, Mwanza, Bukoba tayari vinapatikana. Mikoa mingine tunakutumia. Karibu sana.
1 comments:
Enter your comment...amen kak
Post a Comment