Ukitaka kujapata ushindi lazima ukubali kupoteza. Hiyo ni mojawapo ya kanuni za mafanikio. Watu wote unaowaona wamefanikiwa ni watu walikubali kupoteza na hatimaye wakaibuka washindi.
Ukitaka kuwa mtu unayetakuwa lazima ukubali kuwa mtu ambaye kabla hujawahi kuwa. Na kuwa mtu ambaye hujawahi kuwa ni lazima ukubali kupoteza.
Je unapoteza nini?
Kuna vitu ambavyo unatakiwa kuvipoteza kama, kama muda, marafiki, pesa na kadhalika. Ikumbukwe kwamba ninaposema kupoteza simaanishi unakiacha kama kisichokuwa na maana.
Mfano: kuhusu kupoteza muda. Ukitaka kufanya mambo yako yaende sawa kabisa lazima ukubali kupoteza muda wa kulala na uanze kuamka mapema. Kulala ni muhimu lakini kuamka mapema ni muhimu zaidi. Nafikiri umepata maana yangu halisi ya kupoteza.
Kama marafiki zako ni watu wasio na mipango na malengo ni lazima uachane nao ili utafute marafiki wapya wenye malengo na mipango. Marafiki watakaokujenga na kukuonesha fursa mpya. Marafiki ambao muda mwingi wanawaza mafanikio na sio wale wanaowaza mipira ya Simba na Yanga kila kukicha. Marafiki wanaofuatilia ligi kuu ya Uingereza utafikiri inawalipa. Hao ni watu wa kupoteza na kujiunganisha na watu wapya. Hata kama ni mtu uliyenaye kwenye mahusiano kubali kumpoteza kama ni mtu anayekurudisha nyuma. Kuna watu wengi wamerudishwa nyuma kutokana na watu walionao kwenye mahusiano.
Kama muda mwingi ulikuwa ukiutumia kutizama TV, kuangalia michezo lazima ubadilike na kuanza kuudhuria semina, kusoma makala mbalimbali kama hii unayoisoma sasa, kusoma vitabu kutaja machache. Hapo umekubali kupoteza muda lakini umeweka muda wako katika mambo yanayokufaa na kukujenga.
Kila jambo Fulani lenye kuhitaji mafanikio pia linahitaji pesa. Lazima utumie kiasi Fulani cha pesa kuwekeza kwenye kitu unachohitaji. Hivyo basi usiogope kupoteza pesa kama una malengo makubwa kama unalenga mafanikio.
Leo hii nataka ufikiri vinginevyo na kuona yakwamba kupoteza ni kitu muhimu sana kwa mtu anayehitaji mafanikio. Kupoteza ni kanuni kwa mtu yeyoyote anayehitaji mafanikio na anayehitaji ushindi.
Usiogope kupoteza, maana kupoteza ni tunu kubwa iliyobeba ushindi.
"Mafanikio yako mikononi mwako."
Ndimi:
Edius Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com
Jipatie kitabu cha Barabara Ya Mafanikio kwa shilingi 6000/= tu. Dar es Salaam, Morogoro, Kagera, Iringa, Mwanza tayari vinapayikana. Mikoani tunatuma pia. Mawasiliano; 0764145476/0625951842
Imani yangu mafanikio ni kitu cha kushirikishana. Mshirikishe pia na rafiki, ndugu au jamaa kile ulichojifunza.
1 comments:
Kweli kabisa
Post a Comment