Wednesday, 6 September 2017

Komaa Mpaka Kieleweke

Kuna msemo wa kiswahili unasema "Maji ukishayavulia, sharti uyaoge." Kwa maana ya kawaida tu tunaweza kusema ukianza kitu Fulani usikubali kukiacha kwa vigingi, milima na matatizo unayokutana nayo.

Watu wengi waliofanikiwa ni watu waliokomalia malengo na kuhakikisha wanayatimiza.

Unahitaji kuwa king'ang'anizi ili uweze kutimiza ndoto na malengo yako.

Usikubali kabisa kusema nimeshindwa na kuacha jambo Fulani maana wanasema "Washindwa huacha mambo Fulani, na washindi ni watu wasiokubali kushindwa." Unaweza kukutana na majaribu, misukosuko ya hapa na pale lakini usiruhusu hata siku moja kusema nimeshindwa.

Edson Thomas alifanya majaribio 1000 bila kufanikiwa kuwasha taa au balbu ya umeme. Zoezi la 1001 ndilo lilifanya na kumsaidia kuwa mgunduzi wa balbu za umeme. Kumbe kukomalia kitu kunalipa.

Unahitaji nguvu na moyo wa ujasiri pale unapokomalia kitu ingawa matokeo ni mabovu. Ingawa muda mwingine matokeo hayaonekani, Kama ukikubali kwenda hatua ya ziada nakuhakikishia ushindi wa hali ya juu sana. Nakubaliana na mtu aliyesema "Hakuna msongamano kwenye maili za ziada."

Moja wapo ya watu ambao pia walikomaa mpaka kikaeleweka ni Michael Jordan yeye anasema "Nilipokuwa shule niliambiwa siwezi kucheza mpira wa kikapu, siwezi kufikiri na siwezi kupiga chenga. Niliamka kila siku saa 11 kamili alifajiri kwenda kufanya mazoezi masaa matatu kila siku kabla hakuchakucha ndipo nilipoenda shuleni. Njiani kulikuwa na mende na panya katika giza lile nilichukua mpira wangu na kwenda uwanjani kila siku huku macho yakilengwa na machozi. Siku moja mchezaji aliyekuwa akicheza timu ya kwanza aliumia kiwiko na hakuweza kucheza hivyo aliniuliza " unaweza kucheza nikamwambia ndio." Wakaniambia ingia uwanjani. Nilichukua mpira nikaanza kuwachenga wachezaji. Mara gafla uwanja mzima ukaanza kunishangilia. Kocha naye akasema itabidi tukutafutie namba katika kikosi cha kwanza."

Michael Jordan ni mtu anayetufunza mengi hasa katika hili ninalolizungumzia Leo. Ili ufanikiwe lazima uwe na moyo wa kusema sikubali kushindwa, mimi ni bora, mimi naweza. Leo hii Michael Jordan analipwa dola Milioni 30 za Kimarekani kutokana na jina lake kutumika kama biashara au brand.

Unaweza ukawa kwako kila siku unaona mvua lakini tambua juu ya mawingu hainyeshagi mvua. Hivo ukitaka kukutana na mahali pasipo na mvua lazima upambane kuhakikisha unafika juu ya mawingu na njia pekee ni kukomaa mpaka kinaeleweka.

Hata kama unaona giza, mbele kuna mwanga. Wajapani wanasema "Anguka Mara saba, simama mara ya nane."

Brian Acton mwanzilishi wa mtandao wa kijamii maarufu kama WHATSAPP. Mwaka 2009 alikataliwa kufanya kazi na kampuni ya YAHOO kama injinia wa kampuni hiyo. Mwaka huo huo pia alikataliwa kuajiriwa na kampuni ya FACEBOOK. Alikwenda na kubuni WHATSAPP mwaka huo huo wa 2009. Mwaka 2014 kampuni ya FACEBOOK iliununua mtandao wa WHATSAPP kwa dola za Kimarekani zipatazo bilioni 2.8 Leo hii ni bilionea. Huyu ni mfano wa watu ambao labda tungesema hawawezi kitu lakini kutokana na hule moyo wa kupigania ndoto zao wamefanikiwa.

Kumbe ukitaka kujihakikishia ushindi unahitaji kuwa mtu unayepambana na kuhakikisha ulichokitaka umekiona.

"Mafanikio yako mikononi mwako."
Ndimi:
 Edius Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com

Jipatie kitabu cha Barabara Ya Mafanikio kwa shilingi 6000/= tu. Dar es Salaam, Morogoro, Kagera, Iringa, Mwanza tayari vinapayikana. Mikoani tunatuma pia. Mawasiliano; 0764145476/0625951842

Imani yangu mafanikio ni kitu cha kushirikishana. Mshirikishe pia na rafiki, ndugu au jamaa kile ulichojifunza.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: