Unapolalamika kwamba huna kiatu kizuri cha kuvaa, kuna mwenzako hana miguu.
Unapolalamika kwamba una nguo nyingi za kufua kuna mtu ana nguo moja anaiita kauka nikuvae.
Unapolalamika kwamba foleni ya magari inakuchelewesha ukiwa unaendesha gari lako, kuna mwingine usafiri wake ni taksi namba kumi na moja (miguu) toka azaliwe wala hata ndoto ya kuwa na gari hana.
Unapolalamika kwamba unavyombo vingi vya kuosha kuna wenzio hata kutumia kijiko hawajui, usiwaambie habari za kisu na uma maana watakuona wewe wa ajabu.
Unapolalamika kwamba shule ngumu, kuna wengi walitamani wapate nafasi kama yako lakini waliikosa.
Mara nyingi tukilalamika huwa tunaangalia asilimia 10 tu ya mambo ambayo hatuna wakati tukiwa na asilimia 90 mikononi mwetu. Lakini wengi huangalia asilimia 10 na hivyo kukosa uwezekano wa kuona fursa ya kufanya mambo makubwa.
Kuna mtu mmoja alikuwa amechoka maisha ni mtu aliyekamilika. Siku moja jumatatu, akiwa anatembea huku akisema siku ile ni siku mbaya sana kwake, alitaka aende kuomba pesa kwa watu ili zimsaidie kujikimu.
Akiwa njiani alikutana na mtu mmoja akiwa hana miguu tena akijisikuma kwenye kibaiskeli chake. Aliposalimiana na yule jamaa alimuuliza: "Habari yako?." Yule kilema alimjibu "Leo ni jumatatu nzuri sana. Najiskia mwenye furaha." Huku akitoa tabasamu kali.
Bwana yule baada ya kuona mtu yule ambaye hana miguu na bado amejawa na furaha isiyo na kifani, alijisemea "Mimi nimebarikiwa zaidi, yanipasa kuwa mwenye furaha zaidi ya mtu yule kwenye baiskeli." Badala ya kuendelea kuwa ombaomba na mtu asiye na furaha Bwana yule alikwenda benki akaomba mkopo, akapewa na kujiajiri. Toka siku ile yule Bwana anasema, "Asingelikuwa mtu yule niliyekutana naye barabarani akiwa hana miguu, wakati Mimi nimekamilika. Leo hii nisingelikuwa hapa."
Tujifunze kutokana na hadithi hiyo hapo juu. Unaweza kuwa unalalamika lakini kumbe umekosa vitu kidogo. Asilimia 10 tu ndiyo unayoikosa na umegeuka kuwa mtu mwenye msongo wa mawazo na mlalamikaji. Hebu kaa chini angalia asilimia 90, hesabu baraka zako, sio balaa zako.
"Mafanikio yako mikononi mwako."
Ndimi;
Edius Katamugora
Mwandishi na Mhamasishaji
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email; ekatamugora@gmail.com
Instagram: ediuskatamugora
Edius Katamugora
Mwandishi na Mhamasishaji
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email; ekatamugora@gmail.com
Instagram: ediuskatamugora
Imani yangu ni kwamba mafanikio ni kitu cha kushirikishana. Mshirikishe na mwenzako kile ulichojifunza.
Jipatie kitabu cha BARABARA YA MAFANIKIO kwa 6000/= tu. Piga; 0764145476/ 0625951842 ujipatie nakala yako.
0 comments:
Post a Comment