Friday, 17 November 2017

Naiona Kesho Yako

Habari za asubuhi mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba u mzima wa afya na umejiweka tayari kutimiza majukumu yako ya Leo. Leo ni siku muhimu, usikubali ipotee. One day can make you grow. Siku moja inaweza kukufanya ukue.

              
   
Leo hii kuna kitu unakifanya kwa bidii na unaweka nguvu kubwa lakini kuna kundi kubwa la watu wanakubeza, wanakukebehi na kukwambia kwamba huwezi kufanikiwa. Ni watu wanaokuchukulia poa.

Usikubali wewe pia kuwa mtu wa kawaida, usikubali kujichukulia poa. Naiona kesho yako yenye furaha tele lakini kesho hiyo itakuja endapo hautakata tamaa na utapiga moyo konde na kuendelea kujituma au kufanya kile unachokifanya.

Watu wanaokupa majina ya kubeza na ya kukurudisha nyuma ipo Siku watawaambia wengine historia ya maisha yako, yaani wanaweza kusema mambo ambayo hata wewe huyakumbuki. Waliokuwa maadui zako ndiyo watageuka mashabiki wako. Usikate tamaa.

Inawezekana watu wanaokuzunguka hawaoni thamani uliyonayo lakini Mimi naona thamani kubwa uliyoibeba ndio maana nimeamua kuandika ujumbe huu.

Ndugu zake Yusufu baada ya kuwaambia kwamba ameota ndoto ya kuwa kiongozi waliishia kumchukia na kumwita "Bwana Ndoto." Inawezekana na wewe umepewa majina ya ajabu ajabu kwasababu tu ya kile unachokifanya.

Wale waliomnunua waliona ni kijana anayefaa kuwa mtumwa.

Mke wa Farao aliona ni boyfriend wa kujivinjari naye lakini Farao aliona kiongozi anayepaswa kuwa msaidizi wake ambaye hatimaye alimfanya kuwa waziri katika nchi ya Misri.

Usikate tamaa ipo siku mambo yatakuwa sawa. Endelea kufanya kile unachokifanya. Usiangalie mahali ulipotoka na mahali ulipo sasa. Angalia utakuwa wapi miaka mitano au kumi ijayo. Mimi binafsi nakuona mbali mtu wangu wa nguvu.

Mwandishi maarufu John Mason aliwahi kusema "You were born original, don't die a copy," akimaanisha ulizaliwa ukiwa halisi, hivyo usife ukiwa bandia. Kuwa original, usikubali watu wakufanye mtu bandia. Usikate tamaa.

"Mafanikio yako mikononi mwako."

Ndimi:
Edius Katamugora
Mwandishi na Mhamasishaji
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com
Instagram: ediuskatamugora

Jipatie kitabu cha Barabara Ya Mafanikio kwa shilingi 6000/= tu. Wasiliana nami kwa 0764145476/ 0625951842.

Imani yangu ni kwamba mafanikio ni kitu cha kushirikishana. Mshirikishe ujumbe huu, rafiki ndugu au jamaa yako wa karibu. Itapendeza sana.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: