Kila kitu unachokifanya kinaanzia kichwani mwako.
Kila kitu unachokifanya ni matokeo ya mawazo yako.
Kila kitu unachokifanya ni matokeo ya mawazo yako.
Ndiyo maana Mahatma Gandhi aliwahi kusema "Ulivyo sasa/leo ni matokeo ya kile ulichokiwaza."
Je mawazo yako ni sahihi?
Je mawazo yako yanakupeleka kule unakotamani kwenda au kufika?
Je mawazo yako ni mawazo chanya?
Je mawazo yako yanakupeleka kule unakotamani kwenda au kufika?
Je mawazo yako ni mawazo chanya?
Hayo ni maswali matatu ambayo Leo hii ningependa ujiulize wewe kama wewe.
Kama jibu lako ni "Ndiyo" nikupe hongera sana na nikusihi uendelee na kuwa na mawazo hayo. Kama jibu ni "Hapana" endelea kusoma makala haya kwani yamekulenga wewe hapo.
Je mawazo yako ni chanya.
Watu waliofanikiwa ni watu wenye mawazo chanya. Hata kama kwenye maisha yao wanaona matatizo makubwa lakini wao huona ni mtihani wa kuufanya na lazima wafaulu maana, "Mungu akikupa mtihani anakupa na akili ya kuufanya."
Badili mawazo kuhusu ndoto zako.
Ukiwa na ndoto kubwa lakini wewe mwenyewe huziamini sio rahisi ndoto zako kukamilika, utajitahidi kadri ya uwezo wako lakini wapi. Hii ni kwasababu akili yako haijaruhusu ndoto yako ifanyike. Badili Leo mtazamo kuhusu ndoto zako na kila kukicha ona kama ndoto zako zimekamilika. Nakubaliana na Napoleon Hill aliyewahi kusema "Chochote ambacho akili inaweza kukiamini, akili inaweza kukizalisha."

Badili mawazo yako kuhusu Jana yako.
Watu wengi wamekuwa wakisumbuliwa na kuwaza ya Jana. Mpendwa msomaji jana haitakusaidia lolote lakini kesho imebeba tunu kubwa ya maisha yako. Usiwaze kuhusu kuzaliwa maskini kwani "Kuzaliwa maskini sio kosa lako. Kosa lako ni kufa maskini," kama anavyosema Bill Gates tajiri namba moja duniani.

Usiwalaumu watu kufanya mambo fulani au kusababisha wewe usifanikiwe, hiyo itakufanya uwe na udumavu wa kuwaza utafanya nini. Watu waliofanikiwa sio walalamikaji. Watu waliofanikiwa hawaangalii Jana zao, wanaangalia wanakwenda wapi.
Badili mawazo yako kuhusu watu watakuonaje.
"Watu watanionaje" ni kitu kilichowafanya watu wengi waache kufanya mambo makubwa na yakuwapa furaha huku wakiogopa watu watawaonaje kama wakianza kuwa wa tofauti kwa kutumia vipaji vyao, kubadili marafiki au kuanzisha biashara Fulani ndogo ndogo.

Ukiendelea kusema "watu watanionaje" wewe siku zote utakuwa mtu wa kushindwa. Hauwezi kupiga hatua yoyote kimaisha.
Kwenye kitabu cha Barabara Ya Mafanikio ukurasa wa 75 nimeandika kanuni ya 20-40-60 ambayo ilianzishwa na muigizaji wa kike toka Marekani anayeitwa Shirley Maclaine.
Kanuni hiyo inasema hivi:
"Ukiwa na miaka 20, muda mwingi huwa unahofia watu wengine wanakufikiriaje."
"Ukiwa na miaka 40, unashtuka na kusema sijali watu wengine wananifikiriaje na wanasema nini kuhusu Mimi."
"Ukifikia miaka 60, unagundua hakuna mtu yeyote anayekufikiria." Kila mtu anafikiria mambo yake.
Ukibadili mawazo yako na kuacha kusema "watu watanifikiriaje au watu watanionaje. Utaibadili dunia yako."
"Mafanikio yako mikononi mwako."
Ndimi:
Edius Katamugora
Mwandishi na mhamasishaji
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com
Instagram: ediuskatamugora
Edius Katamugora
Mwandishi na mhamasishaji
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com
Instagram: ediuskatamugora
Imani yangu ni kwamba Mafanikio ni kitu cha kushirikishana. Washirikishe wenzako kile ulichojifunza.
Jipatie kitabu cha Barabara Ya Mafanikio kwa shilingi 6000/= tu. 0764145475
0 comments:
Post a Comment