Monday, 6 November 2017

Ukweli Kuhusu Masaa 10000

Kwenye kitabu chake cha Outliers, Mwandishi Maxwell Gladwell aliandika kuhusu masaa 10000 ambayo wataalamu wa mambo ya mambo ya ubongo husema ni muda unaohitajika ili mtu aweze kuwa amebobea kwenye fani flani.

Kama ni mwandishi, mwanamuziki, mwanamitindo, mchezaji, mwanamahesabu, mkemia na hata jambazi sugu unahitaji masaa 10000 ili uwe umebobea katika kitu unachokifanya.

                               

Ni kweli ni lazima masaa yote 10000?

Ukichukua masaa matatu kufanya kitu unachokifanya kila siku, tuseme mchoraji utahitaji jumla ya miaka Tisa ili kuwa mtaalamu katika fani ya uchoraji.

Watu wengine baada ya kwenda mbali zaidi waligundua yakwamba masaa 10000 yanaweza kubadilishwa na kuwa masaa 20 tu. Yaani ukichukua muda wa masaa ishirini na kuweka nguvu katika kile unachokifanya bila kujisumbua/kujishughulisha na kitu chochote unaweza kuwa mtaalamu mzuri bila hata ya kutumia masaa 10000.

Spidi ni muhimu zaidi ya masaa 10000.
 
Watu wanaofanya mambo kwa spidi wameonekana kufanikiwa zaidi ya wale wanaotumia masaa 10000 au masaa mengi. Hivyo huhitaji masaa mengi ili uwe mtaalamu bali spidi yako ndiyo itakusaidia kufanikiwa zaidi.

Watu wanaojifunza kila siku na kufanyia mambo wanayojifunza kwa haraka zaidi wanafanikiwa haraka sana kuliko wale wanaofanya kwa kuangalia masaa.

Leo hii ndiyo maana unakuta watoto wadogo wanafanya mambo makubwa ambayo hata watu wazima hawawezi kuyafanya na wamefanikiwa vilivyo. Hawa kinachowasaidia zaidi ni spidi yako ya kufanyia kazi vipaji na vipawa walivyonavyo. Ukimuona Naomi Peller mtoto wa miaka 11 akiimba wimbo wake wa BELIEVE ambao ametumia maneno ya Napoleon Hill "Whatever the mind can conceive and believe, the mind can achieve." unaweza kufikiri ni mtu mwenye umri kama Dr. Jazz aliyeimba wimbo wa "Imperfect Life"

Kumbe ukitaka kufanikiwa haraka jitahidi ufanye kwa spidi na sio kwenda na masaa. Ukisubiri masaa wanaofanya kwa spidi utaona wanafanikiwa na wewe unabaki kushangaa. Fanya mambo kwa kasi ya haraka usisubiri kesho wala kesho kutwa. 

"Mafanikio yapo mikononi mwako."

Ndimi:
Edius Katamugora
Mwandishi na Mhamasishaji
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com
Instagram: ediuskatamugora

Jipatie kitabu cha Barabara Ya Mafanikio kwa bei ya shilingi 6000 tu. Tuwasiliane: 0764145476
0625951842.

Wahirikishe marafiki zako kile ulichojifunza.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: