Miezi miwili iliyopita mtaalamu mmoja wa uchumi alibadilisha maisha yangu. Ni aibu kwamba sijawahi kumnunulia hata kinywaji. Mpendwa Vilfredo aliyefariki karibia miaka 100 iliyopita.
Vilfredo Pareto alikua ni mtaalamu wa uchumi na mambo ya saikolojia aliyeishi kuanzia mwaka 1848 hadi mwaka 1923. Amesomea uhandisi akijihusisha na mambo ya uchimbaji wa makaa ya mawe, baadaye alikuwa Mwenyekiti wa mambo yanayohusu siasa za kiuchumi katika chuo cha Laussine kilichopo nchini Switzerland.
Vilfredo Pareto anajulikana kwa kuwa na kanuni inayoitwa "Kanuni ya Pareto." Au maarufu kama 'kanuni ya 80/20'.
Baada ya kutumia fomula zake za kimahesabu, Pareto alifundua kwamba 80% ya utajiri wa jamii Fulani inamilikiwa na 20% ya jamii hiyo. Baadaye kanuni hii ilitumika nje ya mambo yanayojihusisha na uchumi na kukuta ikitumika kila mahali.
Asilimia themanini ya mapeasi kwenye bustani ya Pareto ilitokana na asilimia 20 ya miti ya mipeasi aliyokuwa ameipanda.
Kanuni ya Pareto kwa kifupi inaweza kutafsiriwa hivi "Asilimia 80% ya matokeo husababishwa na Asilimia 20% ya kile ulichokuwa unakifanya."
Unaweza kuitumia Kanuni ya 80/20 kama ifuatavyo pia.
80% ya matokeo hutokana na 20% ya juhudi na Muda.
80% ya mauzo hutokana na asilimia 20 ya wateja.
80% ya muda unaopoteza kwenye simu yako hutokana na asilimia 20 ya applications zilizokwenye simu yako.
80% ya mtizamo chanya uchangiwa na asilimia 20 za ujuzi linapokuja suala la ajira.(Hapa mwajiri ataangalia mtu mwenye mtizamo chanya)
80% ya hisa za uwekezaji humilikiwa na asilimia 20 ya wawekezaji.
Listi inaweza kuwa kubwa sana lakini baadhi ya watu wamekwenda mbali zaidi na Kutengeneza kanuni zenye 90/10, 95/5 na 99/1 ambayo utakisika watu wakisema "Ukitaka kuwa 1% Fanya mambo ambayo 99% hawayafanyi.'' Lakini kanuni ya 80/20 ndiyo hutumika sana.
Nilijuta sana kuifahamu kanuni hii nikiwa nimechelewa lakini nafurahi baada ya kuanza kuitumia katika nyanja mbalimbali imeniletea matokeo makubwa sana na ya tofauti.
Ukitaka kuifahamu fika kanuni hii jiulize maswali yafuatayo;
1. Ni 20% ya vitu gani vinavyosababisha 80% ya matatizo na pia kunifanya kutokuwa na furaha?
2. Ni 20% ya vitu gani vinavyosababisha 80% ya mambo niliyoyatarajia na kunipatia furaha?
Ukiweza kuyajibu maswali hayo mawili vizuri utakuwa mtumiaji mzuri wa kanuni hii na utaona mabadiliko makubwa sana.
" Mafanikio yako, mikononi mwako."
Ndimi
Edius Katamugora
Mwandishi na Mjasiriamali
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
ekatamugora@gmail.com
Edius Katamugora
Mwandishi na Mjasiriamali
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
ekatamugora@gmail.com
Washirikishe marafiki zako kile ulichojifunza. Imani yangu ni kwamba mafanikio ni kitu cha kushirikishana.
0 comments:
Post a Comment