Monday, 18 December 2017

Njia Mbili Unazoweza Kuzitumia Kuelewa Mambo Haraka

Mwalimu wangu mmoja wa sekondari wakati tukiwa kidato cha kwanza alipenda sana kutuambia sisi wanafunzi wake msemo uliosema "Repetitio est mater studiorum."  akimaanisha "Marudio ni mama wa kusoma." 

                          


Ukweli huu nimekuwa nikiuona mara kwa mara wakati ninapokuwa nikisoma. Ukirudia kitu unaupa ubongo nafasi ya kukishika kwa makini.

Kuna njia ambazo unaweza kuzitumia kuongeza uelewa wako haraka sana.

Njia hizo ni kama zifuatazo;

Njia ya sauti (Audio);
 
Imewahi kutokea kwako ukiupenda wimbo Fulani mpya, ambao umetoka siku hiyo hiyo unaweza kuuweka kichwani na kuanza kuuimba utafikiri umeutunga wewe!

Hali hii hutokeaje?
Hali kama hiyo hutokea ukiusikiliza mara nyingi kadri uwezavyo. Ndipo unapopata nafasi ya kuushika vizuri wimbo huo.

Njia ya sauti hutumikaje katika kuongeza uelewa?
Hapa unatakiwa kurekodi Yale mambo uliyojifunza na kisha kuyasikiliza kila mara. Hii itakusaidia pia kutopoteza muda mwingi. Ukizingatia binadamu hupoteza muda wa muhula mmoja wa mwanafunzi (sawa na wiki 16) ndani ya mwaka mzima akiutumia katika kutembea. Kama anavyosema Brian Tracy.

Kumbuka unatakiwa kujirekodi kwa spindi ndogo sana ili uweze kuelewa vizuri. Unaweza kurekodi pia ukiwa na muziki kwa mbali.

Njia ya video:
Kuna watu waliwahi kusema "Kuona ni fahari ya macho." Unapoona kitu katika vitendo unaelewa zaidi. Kwa njia hii unaweza kutizama video za YouTube ili kuongeza uelewa wako na kujifunza zaidi. Bahati mbaya watu wengi wanautumia mtandao wa YouTube vibaya, wanapenda kuona mambo ya starehe hawapendi kabisa kujifunza. Anza leo kujifunza kupitia video utaelewa kwa mapana zaidi. Kama kitu hukielewi ingia YouTube tazama kinavyoelezwa.

"Mafanikio yako, mikononi mwako."

Ndimi;
Edius Katamugora
Mwandishi na Mhamasishaji
0764145476
0625951842

Imani yangu ni kwamba mafanikio ni kitu cha kushirikishana. Washirikishe na wenzako kile ulichojifunza.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: