Tarehe 2 mwezi Desemba mwaka huu 2017 rafiki yangu Saada Mpandachalo (canju_motivational_pilot) aliandika maneno yafuatayo kwenye ukurasa wake wa Instagram:
"Hauhitaji tarehe mosi Januari kubadilisha maisha yako."
Binafsi nilifurahisha na maneno hayo na ni maneno yanayohamasisha lakini pia yaliyoandikwa kutokana na fikra kubwa yenye ubunifu ndani yake.
Watu wengi wanaona hadi Leo hii mwaka 2017 umekuwa mwaka wa matatizo wameupa jina baya "Sitakusahau 2017" si kwa mazuri ila kwa matatizo yaliyowatokea.
Inawezekana na wewe ni mmojawapo wa watu wanaoomba mwaka huu uishe na tuanze mwaka mpya mwaka ambao kwako unauona ni mwaka wa neema.
Ukweli ni kwamba mwaka mpya hautabadili chochote kwenye maisha yako labda kitakachobadilika ni tarehe, mwezi na mwaka. Ni kweli hautawahi kuiona tena 2017 lakini ukweli mchungu ni kwamba umekubali kudanganyika kirahisi, umekubali kudanganywa na mwaka mpya.
Wakati mwaka unaanza kuna watu walikuwa na malengo makubwa kuna watu walikuwa na ndoto kubwa lakini Leo hii wameachana nazo kutokana na matatizo madogo madogo. Basi wameuona mwaka huu kama haufahi na wanategemea kufanya vyema mwaka ujao. Kama wewe ni mmoja wao umejidanganya. Jambo la msingi ni kukubali kutatua matatizo yaliyojitokeza na utakuwa mshindi. "Hauhitaji Januari mosi kubadili maisha yako." Anatuhasa Saada.
"Miaka mizuri sana ya maisha yako ni ile ambayo uliamua kuwa matatizo ni yako Kwa matatizo yako humlaumu mama yako, mazingira au rais. Unatambua kuwa unatiisha mwelekeo wa maisha yako." Alisema Albert Ellis mwanasaikolojia wa kimarekani.
Jitahidi utatue matatizo yako na sio utumie kigezo cha mwaka mpya kufanya uyakimbie. Ukweli ni kwamba matatizo hayakimbiwi. Ukiyakimbia yatakukimbiza na kamwe huwezi kuwa mshindi lazima yakushinde. "Wakati wowote maisha yanapodondosha pini na sindano kwenye njia yako, usikae mbali. Badala yake usikae mbali ili pini zilezile zisikuumize tena." Alisema Sariajy Rathi.
Uchunguzi unaonesha kwamba, malengo mengi ya watu hufa wiki ya pili ya mwezi Februari. Yaani wanaanza mwaka na motisha kubwa juu ya doto na malengo yao lakini baadae ndoto zao huyeyuka kama mshumaa. Usikubali kuwa mmoja wao hao walidanganyika na Januari mosi. Jitahidi sana uhakikishe malengo uliyojiwekea mwaka huu umeyatimiza wala usiyaache nusu nusu, yatimize kwanza ndipo uanze kufanyia kazi malengo mapya.
"Njia pekee ya kumla chura ni kumtafuna mzima mzima." Alisema Brian Tracy mwandishi wa Vitabu akitaka kutukumbusha kuhakikisha tunatimiza lengo moja baada ya jingine.
Kumbuka:
Usikubali kudanganyika na mwaka mpya. Hauhitaji Januari mosi kubadili maisha yako.
Usikubali kudanganyika na mwaka mpya. Hauhitaji Januari mosi kubadili maisha yako.
Ndimi;
Edius Katamugora
Mwandishi na Mhamasishaji
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com
Instagram: ediuskatamugora
Edius Katamugora
Mwandishi na Mhamasishaji
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com
Instagram: ediuskatamugora
Jipatie kitabu cha Barabara Ya Mafanikio kwa shilingi 6000 tu.
Imani yangu ni kwamba Mafanikio ni kitu cha kushirikishana. Mshirikishe na mwenzako kile ulichojifunza.
0 comments:
Post a Comment