"Wakati/muda unapochukua maamuzi magumu. Utasikia wakisema. Amerukwa na akili. Ni kichaa. Amechanganyikiwa. Maneno kama hayo yasikukatishe tamaa. Songambele."~Edius Katamugora ~
Baba wa uchimbaji mafuta Edwin L. Drake aliambiwa mwaka 1859. "Unataka kuchimba mafuta utakuwa umerukwa na akili! Kilichofuata ni historia bwana huyo hakusikiliza maneno ya kukatisha tamaa.
Leo hii mafuta aliyoyagundua bwana Edwin L. Drake ndiyo yanayofanya magari yetu yatembee, pikipiki, bajaji, ndege, meli na hata boti.
Viwanda mbalimbali vinaendesha mitambo mitambo yake kwa kutumia mafuta. Leo hii watu wanasomea mambo yanayohusu uchimbaji wa mafuta ili baadae wawe wahandisi wa mafuta(petroleum Engineers). Inawezekana bila kuwepo kwa mafuta mambo mengi yasingefanyika kama yanavyoonekana leo hii.
Plastiki nyingi zinatengenezwa kutokana na vitu vinavyotokana na uchimbaji wa mafuta ya Petroli.
Baada ya kugundulika kwa mafuta nchini Uganda, sasa linajengwa Bomba la mafuta kutoka Uganda kwenda bandari ya Tanga, Tanzania. Watu wengi watafaidika kutokana na ujenzi huo wa bomba la mafuta.
Mataifa mengi duniani leo hii yanaongoza kwa kuwa na uchumi mkubwa kwasababu ya uuzaji wa mafuta yanayochimbwa katika nchi zao.
Watu wengi wamekuwa matajiri wakubwa duniani kwa kumiliki visima vya mafuta, akiwemo Tajiri namba moja Afrika, Aliko Dangote.
Wengine wamekuwa wafanyabiashara wakubwa nchini kupitia uuzaji wa mafuta ambayo wanamiliki sheli za mafuta zisizo na idadi hapa nchini.
Haya yote yametendeka baada ya Bwana Edwin L Drake kuwa na nia ya dhati ya kutaka kuchimba mafuta na kuchukua maamuzi magumu ingawa aliambiwa amerukwa na akili.
Wakati nikiwa naandika kitabu changu cha Barabara Ya Mafanikio kuna mtu alinikuta mezani nikiwa katika harakati za uandishi wa kitabu hicho. Nilimwambia kwamba naandika kitabu, akaniambia "Dogo umekuwa kichaa." Maneno yale yaliniumiza sana lakini nilijua ninachokitaka, sikukata tamaa niliendelea kuandika hadi nikafikia hatua ya kukichapa.
Leo hii kitabu cha *Barabara Ya Mafanikio* kimekuwa alama kubwa kwangu. Kimekuwa fursa inayofungua milango ambayo kila kukicha naona ni miujiza kwenye maisha yangu.
Inawezekana hata wewe ndugu yangu uliamua kuanza kufanya kitu fulani watu wakasema umerukwa na akili, wewe ni kichaa, umechanganyikiwa, kutaja machache. Maneno kama hayo hayapaswi kukurudisha nyuma. Maana wahenga walisema ```penye nia pana njia```. Kuwa mtu Mwenye nia ya dhati.
Watu wakikurushia maneno ya kukatisha tamaa hakikisha hayawi breki kwenye Barabara yako ya mafanikio. Maneno ya kukatisha tamaa yakuongezee spidi ya kufanya kwa ufanisi zaidi.
*Mafanikio yako, mikononi mwako.*
Ndimi;
Edius Katamugora
Mwandishi na mhamasishaji
0764146476
0625951842 (WhatsApp)
Www.bideism.blogspot. com
Email: ekatamugora@gmail.com
Edius Katamugora
Mwandishi na mhamasishaji
0764146476
0625951842 (WhatsApp)
Www.bideism.blogspot. com
Email: ekatamugora@gmail.com
JIPATIE KITABU CHA BARABARA YA MAFANIKIO KWA SHILINGI 6000 TU.
0 comments:
Post a Comment