Steven K.
Scott aliwahi kusema “Kompyuta yenye
nguvu kubwa sana sio ile unayoiona kwa
macho ikiwa imefungiwa kwenye fremu Fulani bali ni kitu kidogo kisichoonekena
kilichofungiwa ndani ya kichwa chako.”
Ubongo wa
kila mwanadamu umeumbwa kwa namna ya ajabu sana, wakati kompyuta ikiweza
kupokea taarifa moja kwa muda Fulani, ubongo wako unawez kupokea taarifa
milioni 4 na kuzifanyia kazi kwa wakati mmoja. Inashangaza kwamba ubongo huo
huo unafanya kazi kwa masaa 24 kila siku, siku sab kwa wiki, kwa miaka 70, 80
na hata 100 bila matengenezo yoyote.
Najaribu
kufikiria hakuna mashine yoyote inayowea kufanya kazi kama ubongo wako
unavyofanya kazi bila kufanyiwa marekebisho au matengenezo yoyote.
Kuna mambo
ambayo unatakiwa kuupatia ubongo wako ili ufanye kazi kwa viwango aya uwezo
wake. Kuna vyakula au vinywaji tunavyokunywa ambavyo vipunguza uwezo wa ubongo
wetu kufanya kazi kwa ufasaha.
Ubongo
wako kama zilivyosehemu nyingine za mwili unahitaji kupata mlo kamili.
Kuna vitu
vitatu vya kuzingatia unapohitaji kuupatia ubongo wako chakula
kitakachohusaidia kufanya kazi vizuri:
1.
Maji 2. Mlo kamili
3 3Kuepuka kuvimbiwa wakati wa kula.
Kitu cha
kwanza muhimu ni kwamba ubongo wako unahitaji kuwa katika hali ya unyevuunyevu
ili ufanye kazi kwa ufasaha. Unahitaji kunywa lita kadhaa za maji kila siku ili
ubongo wako ufanye kazi kwa ufasaha.
Ili zege
iwe imara inahitaji kuwa katika hali ya unyevuunyevu ndipo itakauka na kuwa
imara Zaidi. Hivyo hivyo ubongo wako pia unahitaji kuwa katika hali ya
unyevuunyevu (uwe na maji) ili ufanye kazi kwa viwango vya juu sana.
Watu
wengi hufanya kazi chini ya uwezo wao
kutokana na kuwa katika hali ya kukosa maji mwilini mwao. Kimsingi tunakosea
sana tunapokunywa naji wakati tunahisi kiu, hiyo inamaana kwamba tayari mwili
wako umekosa maji kwa muda mrefu. Kitaalamu unashauriwa kunywa glasi mbili au
tatu za maji kila unapoamka maana ubongo wako hufanya kazi nyingi wakati wa
usiku unapokuwa umelaala hivyo unakuwa umepoteza maji mengi.
Kwa mujibu
wa (H.H Mitchel, Journal of biological Chemistry 158) asilimia 73 ya ubongo na
moyo ni maji na mapafu yan asilimi 83 ya maji, ngozi ina asilimi 64 ya maji,
misuli na figo vina asilimi 75 na mifupa ina asilimia 31. Kumbe sehemu kubwa ya
mwili wa mwanadamu ni maji.
Uchunguzi
uliofanywa na Trevor Brocklebank katika chuo cha Leeds huko Uingereza uligundua
kwamba wanafunzi waliopata matokeo mazuri darasani ni wale waliokunywa karibia
glasi nane za maji kila siku.
Mtunzi na
mwandishi wa kitabu cha Mbinu 7 Za Kupata
Mafanikio Halisi, Aderitus Ngimbwa ametoa ushauri mzuri unaoweza kutujengea
kuwa na utaratibu wa kunywa maji kila siku.
Bwana
Aderitus anasema;
- · Usisubiri uwe na kiu ndo unywe maji.
Unapoamka asubuhi kunywa maji, baada ya kula kunywa maji, kunywa
maji ukimaliza kufanya mazoezi,
mezani kwako iwepo chupa ya maji na kazini kwako usisahau kubeba chupa ya maji.
·
- Weka kengele ya kukumbusha(alarm) na andika mahali.
Tumia
simu au kompyuta yako kuweka kengele ili ikukumbushe kunywa maji baada ya kila
muda Fulani. Andika mahali kwenye kitabu chako cha kumbukumbu (notebook) au
karatasi utakayoisoma mara kwa mara na kukumbuka tabia yako mpya ya kunywa
maji.
Pili,
unahitaji kula mlo kamili. Kila aina ya chakula unachokula kinaleta matokeo
Fulani mwilini. Vyakula vyenye Protini kama vile mayai, maziwa, samaki na kuku
hutengeneza kemikali a,bazo husaidia ubongo kufanya kazi vizuri Zaidi. Vyakula vyenye wanga kama vile
mboga za majani, wali na matunda hutengeneza kitu kinachoitwa amino acid tryptophan hushusha uwezo wa
ubongo kufanya kazi vizuri.
Vinywaji
kama kahawa na chai huufanya ubongo ufanye kazi vizuri kwa muda mfupi tu ndiyo
maana muda mwingine ukinywa kahawa unakosa usingizi. Kunywa kahawa nyingi
husababisha kizunguzungu, maumivu ya kichwa na kupunguza usikivu na
ufatiliaji(concentration). Kahawa pia ni kinywa kinachofyonza maji mengi
mwilini. Ukinywa kikombe kimoja cha kahawa unahitaji vikombe viwili vya maji.
Pombe pia hupunguza uwezo wa kufikiri na
hufyonza maji mengi mwilini ndiyo maana mtu aliyekunywa pombe nyingi usiku wa
jana huamka asubuhi inayofuata akiwa na uwezo duni wa utendaji kazi.
Wote
tunahitaji kula mlo kamili lakini tukumbuke kupunguza matumizi ya vyakula
vyenye mafuta, wanga kupita kiasi, chumvi, sukari, kunywa kahawa na pombe
kupita kiasi kwani vitu hivyo vinaathiri uwezo wa ubongo kufanya kazi kwa
ufasaha.
Kitu cha
tatu na cha mwisho ni kuwa na kiasi katia kula, ukila chakula kingi mfumo wako
wa mmeng’enyo hufanya kazi kubwa sana kuchukua damu yenye oksijeni, ndiyo maana
baada ya kula chakula kingi huwa tunahisi usingizi: Kwasababu ubongo wako
unakosa damu itakayoufanya ufanye kazi kw ufasaha. Kumbuka unapokula usile
ukavimbiwa, kula chakula cha wastani.
"Mafanikio yako, mikononi mwako."
Ndimi
Edius Katamugora
Mwandishi na Mhamasishaji.
0764145476
0625951 842(WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com
JIPATIE KITABU CHA BARABARA YA MAFANIKIO KWA SHILINGI 6000 TU. POPOTE ULIPO UNATUMIWA. PIGA 0764145476
WASHIRIKISHE NA MARAFIKI ZAKO KILE ULICHOJIFUNZA KWANI MAFANIKIO NI KITU CHA KUSHIRIKISHANA.
0 comments:
Post a Comment