Tuesday, 6 March 2018

Kutoa Ni Moyo Vidole Huachia

Zig Ziglar mwandishi na mhamasishaji maarufu aliwahi kusema "Utapata chochote unachokitaka kwa kuwasaidia wengine kupata wanachohitaji." Naye Albert Einstein alikuwa na haya ya kusema "Nimefika hapa nilipo kwa kusimama kwenye mabega ya watu wengine."

Hakuna furaha kubwa sana kama kuwasaidia watu wengine kupata wanachohitaji. Kutoa ni moyo, vidole huachia. Unapowasaidia wengine kuna furaha ya ajabu ambayo hutokea pale unapowasaidia wengine.

Haupungukiwi chochote kumsaidia Dada/kaka wa nyumbani kuosha vyombo ulivyotumia kulia.

Haupungukiwi chochote anapowavusha watoto wadogo Barabara ili wawahi shuleni.

Haupungukiwi chochote endapo utamfundisha rafiki yako mambo ambayo hayaelewi darasani.

Haupungukiwi chochote endapo utamsaidia mfanyakazi mwenzako kazi zake ingawa muda wako wa kufanya kazi tayari umekwisha.

"Ingekuwaje kama kila mtu angejitoa na kuwa mzuri kila siku? Fikiria ofisini, shuleni na nyumbani."- Anasema Joel Osteen, mchyngaji na mhamasishaji.

Ni kweli dunia ingekuwa mahali pa furaha kama kila mtu angejitoa kwa ajili ya watu wengine. Kila siku hakikisha kuna kitu umefanya kuwasaidia wengine. Katika kuwasaidia wengine tunakua zaidi. Mfano mwanafunzi anayemfundisha mwanafunzi mwenzake hujua zaidi katika kusaidia huko.

Ukitaka furaha ya SAA moja. Lala.

Ukitaka furaha ya siku moja. Nenda kavue samaki.

Ukitaka furaha ya mwezi mmoja. Oa au Olewa.

Ukitaka furaha ya mwaka mmoj shinda bahati nasibu.

Ukitaka furaha ya maisha yako yote. Jitoe kwa ajili ya wengine, kuwa mwema na mzuri kwa ajili ya watu wengine.

" Mafanikio yako mikononi mwako."

Ndimi:
Edius Katamugora
Mwandishi na mhamasishaji.
0764145476
0625951842 (WhatsApp).
Email: ekatamugora@gmail.com

Imani yangu ni kuwa Mafanikio ni kitu cha kushirikishana. Washirikishe na marafiki zako ujumbe huu.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: