Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba u mzima na unaendelea na majukumu yako vyema kabisa.
Ni siku nyingine ambayo tunapata nafasi ya kujifunza kitu kipya kwani kujifunza siku zote akuishi.
Naam.... Makala hii ni maalumu kwa wanavyuo wote ambao wameanza likizo yao siku za karibu lakini pia na wale wanaotarajia kuanza likizo yao hivi karibuni.
Kwanza niwape pole na masomo na niwapongeze sana kwa kuweza kumaliza Muhula wa kwanza ni jambo la kushukuru Mungu.
Wakati wa likizo ni wakati ambao ukiweza kuutumia vizuri utaweza kupata matokeo chanya ambayo kesho na kesho kutwa yataleta mchango mkubwa kwenye maisha yako.
Leo hii nimekuandalia mambo baadhi ambayo unatakiwa kuyafanya wakati wa likizo yako na nakuhakikishia likizo yako itakuwa poa kabisa.
Mambo ambayo unatakiwa kuyafanya wakati wa likizo:
1.) Fanya Tafakari/Tahajudi (Meditation).
Unahitaji kuwa na muda wa pekee na kwenda sehemu iliyotulia (ukiweza nenda garden yeyote (green areas) maana wanasaikolojia wanasema ni nzuri kwa tafakari maana inaendana na asili na humfanya mtu kujisikia vizuri) kisha Fanya tafakari kuhusu muhula ulioumaliza.
Jichunguze ulifanya vizuri wapi lakini pia ulifanya vibaya wapi.
Maswali ya kujiuliza hapa katika tafakari yako;
i). Ni tabia gani ambazo natakiwa kuziacha ambazo baadae zitakuja kuathiri maisha yangu?
i). Ni tabia gani ambazo natakiwa kuziacha ambazo baadae zitakuja kuathiri maisha yangu?
ii). Ni tabia gani mpya natakiwa kuzianzisha?
iii). Ni mambo gani yamekuwa yakinipotezea mwelekeo na yanayopoteza muda wangu?
iv) Ni mambo gani mazuri nimeyafanya katika muhula huu na nahitaji kufanya zaidi ya hapo?
Hayo ni baadhi ya maswali unayoweza kujiuliza pamoja na mengine mengi. Kumbuka kuyaandika yote hayo kwenye notibuku yako maana huwezi kukumbuka kila kitu baada ya muda Fulani. Siku moja mhamasishaji Zingo The Greatest aliwahi kuandika makala akisema, "Kocha akitoa kadi anaandika, sisi tukitumia pesa tunaandika kichwani." Akitaka kuonesha umuhimu wa maandishi.
2.) Soma vitabu;
Hapa siongelei vitabu vya darasani bali naongelea vitabu vinavyoongelea maisha ya kila siku ya mwanadamu anayetaka kufanikiwa (self help books). Muhula mzima umekuwa ukisoma vitabu vya darasani na madesa. Muda wa likizo utumie kusoma vitabu nje ya chuo.
Mtu yeyote anayetaka kufanikiwa katika kitu anachokisomea lazima awe mtu mwenye maarifa na maarifa yanapatikana vitabuni. Katika kusoma vitabu watu wengi wamebadilisha maisha yao.
Siku moja Og Mandino(mwandishi wa kitabu cha The University Of success) akiwa amekata tamaa na maisha akachukua maamuzi magumu ya kujiua. Kabla ya kufanya kitendo hicho alichukua kitabu cha Think And Grow Rich na baada ya kukisoma alibadilisha maamuzi yake. Ndipo alipoandika kitabu cha "The Biggest Sales." Kilichomfanya awe muuzaji bora wa vitabu "Best seller."
Inawezekana na wewe unakumbana na changamoto nyingi lakini hujui kwamba kuna vitabu tayari vimeandikwa kuhusu changamoto unayoipitia Leo hii ni wewe tu kuchukua hatua na kusoma Vitabu hivyo.
Ifuatayo ni orodha ya vitabu vitano ambavyo kila mwanachuo inabaidi asome kabla ya kuingia mtaani:
1). Why 'A' students work for 'C' students and Why 'B' students work for government- Robert Kiyosaki.
2). How to influence people and win friends- Dale Carnegie
3). Rich Dad, Poor Dad- Robert Kiyosaki
4). Think and Grow Rich- Napoleon Hill
5). The Magic of Thinking Big- Robert Schwartz
Ukivikosa nicheki WhatsApp 0625951842 nikusaidie namna ya kuvipata.
3). Weka malengo:
Unahitaji kukaa chini na kuweka ni malengo gani unatakiwa kuyafikia hasa kitaaluma kwa muhula ujao. Kumbuka kwenye kuweka malengo hakikisha unaweza malengo ya juu sana. Watu wengi hufeli kwasababu wanaweka malengo ya chini na wanashindwa kufikia hata hayo waliyoyaweka. Maana akili siku zote hufanyia kazi kile kitu ulichokipanga. Maana hata Mithali inasema "Jinsi mtu anavyofikiri, ndivyo alivyo."
Kuna mtu mmoja aliwahi kusema "Lenga mwezi, ukiokosa unaweza kuanguka kwenye nyota moja wapo. Ukilenga nyota ukianguka utakosa hata mahali pa kutua."
4).Jifunze Kitu ulichokua unatamani kujifunza nyuma;
Kama kuna mambo ulikuwa ukipanga kuyafanya huko nyuma muda muafaka ni sasa. Watu wengi wanapenda kujifunza mambo lakini hawachukui hatua. Ukitaka kutoka kwenye kundi la watu wa namna hiyo anza kuchukua hatua. Usiseme kesho maana Benjamin Franklin aliwahi kusema "Kama kuna kitu unaweza kukifanya Leo kifanye, kesho unaweza kuwa umechelewa."
Kumbuka pia dunia inabadilika kwa kasi sana kila kukicha mambo mapya yanakuja hivyo spidi yako ya kujifunza mambo inatakiwa kuwa ya hali ya juu sana. Hakikisha kiu yako ya kutaka kujifunza haikati.
5) Anza kuwekeza;
Wengine ndio wakimaliza muhula ujao tayari mtaa unawaita. Hamna bumu tena, hamna pesa ya matumizi uliyokuwa ukipewa. Haya huwa nayaita "Maisha baada ya bumu!." Ulishawahi kujiuliza ukimaliza chuo utakuwa na vyanzo vipi vya pesa?.
Njia rahisi ni kuanza kuwekeza kwenye pesa kidogo kidogo unayoipata. Pesa kidogo kidogo unayoiweka Leo kesho itakusaidia. Kumbuka kuvaa na kula aviishi. Ni bora ukaumia Leo chuo kuliko kwenda kuumia mtaani.
Unaweza sema huna pesa lakini kuna watu ambao nawajua walioweza kuanzisha makampuni makubwa kwa pesa waliokuwa wakitunza wakati wakiwa wanasoma chuo.
6). Kwa wanaopata nafasi ya kusafiri;
Ukipata nafasi ya kubadili mazingira usiwaze tu kula bata. Katika mazingira unayopita kifunze tamaduni mbalimbali za watu. Angalia ni fursa gani zinazofanyika ulipo na hujawahi kuziona maeneo mengine. Huenda fursa hiyo ndiyo itakutoa baada ya chuo. Waswahili hawakukosea waliposema "Tembea uone."
"Mafanikio Yako Mikononi Mwako."
Ndimi:
Edius Katamugora
Mwandishi na Mhamasishaji
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com
Edius Katamugora
Mwandishi na Mhamasishaji
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com
Jipatie kitabu cha "Barabara Ya Mafanikio" kwa shilingi 6000/= tu. Piga 0764145476
Imani yangu ni kwamba Mafanikio ni kitu cha kushirikishana. Mshirikishe na rafiki au ndugu yako makala hii.
0 comments:
Post a Comment