Tuesday, 13 March 2018

MAMBO MUHIMU YA KUFAHAMU KUHUSU BIASHARA



                  Image result for business

Anza na soko dogo:

Biashara nyingi zilizofanikiwa zilianza kwa kuuzia soko dogo na baadae kupanuka. Huwezi kumudu kulihudumia soko kubwa kama soko dogo limekushinda kulihudumia. Hata mtoto huanza kwa kutambaa na si kwamba anazaliwa tu na kuanza kutembea siku hiyo hiyo. Biashara ipo hivyo hivyo lazima huanze kwa kulihudumia soko dogo linalokuzunguka.

Facebook iliyoanziashwa na mwanafunzi wa chuo kikuu cha Havard Mark Zuckerberg ilianzishwa ilikuwaunganishwa wanadarasa wenzake pamoja na si kuiunganisha dunia nzima. Jeff Bezos alianza stoa ya Amazon kwa dhumuni la kuuza vitabu, leo hii Amazon inauza vitu tofauti tofauti mbali na vitabu.



Ukiwa ndani ya Biashara usishindane bali toa huduma na bidhaa bora:

Kushindana katika biashara si tija maana wakati mwingi utabaki kutizama mshindani wako anafanya nini na huku husongi mbele.
Ukikazana kushindana utajikuta hutoi bidhaa na huduma bora na hivyo mauzo yako kushuka na hatimaye unaweza kushindwa biashara. Mwaka 2010 makampuni ya Google na Microsoft kila moja lilikuwa likiizidi kampuni ya Apple kiasi cha pesa walizomiliki kutokana na biashara kampuni hizo zilizozifanya.
Mwaka 2013 kampuni ya Apple ilizishinda kampuni zote mbili kwa kipato. Apple ilimiliki kiasi cha dola za Kimarekani zipatazo bilioni 500 huku Google na Microsoft zikimiliki zote kwa pamoja dola za kimarekani bilioni 467.

Wafuate watu kwenye mitandao wanayoitumia:

Kama marafiki zako na wateja wengi wa bidhaa zako kwenye mitandao Fulani hakikisha na wewe umejiunga na mitandao hiyo.
Kama wateja na marafiki zako wamejiunga na facebook au Instagram hakikisha na wewe umejiunga katika mitandao hiyo. Ukishindwa kufanya hivyo biashara yako itafeli. Kuna msemo unasema “Wanunuaji huenda kule wauzaji waliko.” Kinyume chake ni sahihi pia.

Tengeneza nidhamu ya kuikuza biashara yako.

Mwanzo nilianza kwa kusema anza na soko dogo lakini kumbuka pia kuwa unahitaji kuikuza biashara zao. Kuna watu toka tunakua hadi leo hii tumekuwa watu wazima biashara zao ni zile zile hakuna kitu walichoongeza wala kuendeleza, hiyo ni hatari sana katika biashara. Biashara inabidi uione kama mtoto kila siku anakua, alianza kwa kutambaa inabidi ifike muda aache kutambaa, aanze sasa kutembea, akifanikiwa akimbie, kutaja machache. Anza kidogo lakini jenga fikra kubwa ya kuipanua biashara yako. Anzia padogo, malizia pakubwa.

Ndimi:
Edius Katamugora
0764145476
ekatamugora@gmail.com

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: