1. Tumia zaidi ya pesa unayoigiza na ikiisha kopa.
2. Tazama movies na series kila siku na hakikisha kila mechi unaangalia.
3. Soma tu yale ya darasani maana ndiyo kazi utakayoifanya maishani.
4. Cheza michezo ya kubahatisha, bet mara nying uwezavyo. Tatu mzuka, Biko na Soka Bet hakikisha unazifanyia kazi.
5. Endelea kulalamikia serikali. Usichoke kusema vyuma vimekaza.
6. Kaa vijiweni unapiga stori na washikaji au mashoga zao. Jiunge na magroup ya Wasap na Facebook na vichekesho na stori.
7. Tafuta marafiki wanaokwenda na wakati. Wewe ni kijana wa DOTCOM bhana. Design mpya za nguo, aina mpya ya simu hakikisha vyote havikupiti.
8. Tumia kichwa chako kunyoa mitindo mbalimbali kama kiduku na pia kusuka mitindo mbalimbali wala usijisumbue kuwaza kibunifu na kuwazia kesho yako.
9. Sambaza na fuatilia umbea mara nyingi uwezavyo. Zile page za Instagram za umbea hakikisha unazifollow zote achana na habari za biashara na ujasiriamali. Hakikisha upo updated.
10. Post picha zako ukila bata katika mitandao ya Facebook na Instagram upate like za kumwaga. Maisha yenyewe mafupu. Wewe kula tu ujana.
11. Usiamke mapema. Unawahi kuamka ili ugundue nini?.
12. Endelea kufanya mambo yanayowafurahisha wazazi wako wakati wewe uyapendi.
Edius Katamugora
0764145476
ekatamugora@gmail.com
0 comments:
Post a Comment