Yusufu alikuwa mtoto wa Yakobo,
akiwa na miaka kumi na saba baba yake alitokea kumpenda sana maana alikuwa ni
mwana wa uzee wake, akamtengenezea kanzu ndefu.
Ndugu zake walipoona anapendwa zaidi
wakaanza kumchukia.
Sikumoja Yusufu akaota ndoto na
kuwaambia ndugu zake, “Tafadhalini, sikieni ndoto hii niliyoiota. Tazama, sisi
tulikuwa tukifunga maganda shambani, kumbe! Mganda wangu ukaondoka ukasimama na
tazama, miganda yenu ikazunguka ikainama mbele ya mganda wangu.
Ndugu zake wakamwambia, “Je, ni
kweli utatumiliki sisi? Wakazidi kumchukia kwa ajili ya ndoto yake na kwa
maneno yake.
Siku nyingine akaota tena ndoto
ambayo ilimwogopesha hata baba yake, maana aliota akiwa kiongozi mkubwa. Ndugu
zake wakazidi kumchukia wakapanga njama ili wamwue.
Kwenye jamii zetu na mazingira
yetu ya kila siku kuna wakina Yusufu wengi. Kuna watu wengi walikuwa na ndoto
kubwa lakini ndoto zao zimezimwa kama mshumaa.
Kuna watu walikuwa na uwezo
mkubwa wa kubadili picha inayoonekana sasa na kuleta picha mpya lakini lakini
wameshindwa kwasababu wameambiwa ndoto zao si za kweli.
Ni mara ngapi umeambiwa maneno
kama haya?:
Kazi uliyochagua sio sahihi.
Masomo unayosomea hayana ajira.
Kipaji ulichonacho akiwezi
kukufikisha popote.
Hauna akili. Wewe ni kilaza.
Hauwezi kufika popote.
Wewe ni mtoto mkorofi, hauna
mbele wala nyuma.
Kuna nyakati zinafika unahitaji
kuwa kama Yusufu.
Watu wanaofanana na Yusufu ni
wale waliombiwa mambo fulani hayawezekani lakini wao wakaziba masikio na
kuendelea kupiga hatua katika hatua ya ziada na kufika mbali maana walijua
hakuna msongamano kwenye hatua ya ziada.
Martin Luther King aliwahi
kusema, “Nina ndoto.” Yusufu alikuwa na ndoto. “Haijalishi unatokea wapi. Ndoto
zako ni za kweli,” ni maneno ya Lupita Nyong’o.
Wanasema ndoto sio unachokiota
wakati umelala. Ndoto ni kile kitu kinachokufanya ukose usingizi. Kwa msingi
huo ukiendelea kulala sio rahisi kutimiza ndoto zako bali ukiamka unaweza
kuzifanya ndoto zako kuwa kweli.
John Paul DeJoria akiwa katika
shule ya upili (Kidato cha tano na sita) mwalimu wake alimwambia hawezi kufika
popote kimaisha. John Paul pamoja na kuhangaika katika katika kutafuta maisha
kuna siku alikumbwa na ukata wa hali ya juu, mke wake aliyekuwa naye akamkimbia
na kumwachia mtoto wa miaka miwili.
Alianza kuokota chupa tupu
zilizotumika na kuziuza ili amtunze mwanae. Siku zote alimwambia mwanae,
“Tutatoka kimaisha pamoja.” Alifanya pia biashara ya kuuza magazeti mlango hadi
mlango.
Ilifika hatua akaamua kuanzisha
kampuni, watu wakamwambia hana elimu yoyote ya biashara na hana pesa za kutosha
za kuendesha biashara. John Paul akaendelea kukomaa.
Mwaka 2015, gazeti la Forbes
lilimtaja kama tajiri namba 234 kati ya matajiri 400 kutoka Marekani akiwa na
utajiri wa dola bilioni 2.8 za kimarekani. Yeye pia ni mwanzilishi wa bidhaa za
nywele zinazojulikana kama Paul Mitchel.
John Paul DeJoria ni Yusufu wa
leo. Kuna haja ya wewe kuamini katika ndoto zako na hakuna mtu atakaye kuja
kufanya ndoto zako kuwa za kweli isipokuwa wewe mwenyewe. “Wakati ujao
unamilikiwa na wale wanaoamini katika uzuri wa ndoto zao.”
Je upo tayari kuishikilia ndoto
yako hata kama hakuna anayeona uwezo ulionao?
Je, upo tayari kuhakikisha ndoto
yako inakamilika hata kama wazazi wako, ndugu zako na hata marafiki zako wa
karibu wanasema hauwezi kufika popote.
Tatizo kubwa linalosababisha watu
wengi kuachana na ndoto zao ni kusikiliza sauti za watu wengine kuliko sauti
zao za ndani. Watu wanaweza kukuchukulia poa lakini wewe ukianza kujichukulia
poa tatizo huanzia hapo. Familia ya Yusufu haikuamini katika ndoto zake lakini
yeye alijiamini.
“Kila ndoto huanza na yule
anayeiota. Kila mara kumbuka kuna nguvu ndani yako, uvumilivu na kiu ya nyota
za kuibadili dunia.” (Harriet Tubman).
Usikubali hata siku moja ndoto
yako izimwe ghafla kama mshumaa. “Kinachonihamasisha ni wale watu wanaoniambia
hauwezi kufanya kitu fulani. Tafadhali niambie siwezi kufanya kitu fulani,”
(Darren Hardy). Yusufu alihamasishwa na maneno ya ndugu zake. Maneno ya
wanaokukatisha tamaa yakupe hasira ya kutimiza ndoto zako na wala si kurudi
nyuma.
"COME AND SEE"
EDIUS KATAMUGORA
0764145476
ekatamugora@gmail.com
UNAWEZA KUPATA VITABU VIFUATAVYO TOKA KWANGU:
1. Barabara Ya Mafanikio 6000/=
2. Namna ya kuwa mtaalamu ukiwa bado unasoma 15000/=
mawasiliano: 0764145476. Karibu sana.
0 comments:
Post a Comment