Ukiendelea kuogopa watu wataseamaje, watu watakuonaje, sijui hawataipokea bidhaa yangu hauwezi kufika popote kwenye biashara.
Ukitaka kujua umekomaaje kwenye mauzo anza kutafuta nafasi ya kupenya na kuwafikia watu ambao hawakujui na hawajawahi kukuona.
Ukiweza kuwauzia bidhaa watu wageni katika uso wako utafika mbali sana kwenye biashara yoyote.
Kumbuka neno "Watu watanifikiriaje." limekuwa chanzo cha watu wengi kuchelewa kufanikiwa.
Watu wote unaowaona kwenye biashara walifikia hatua wakasema sijali watu watanionaje au watasemaje lazima nifanye hii biashara.
Biashara inahitaji ujasiri, ukiwaogopa watu umewaogopa wateja, umepishana na pesa.
Wafuate watu walipo, waoneshe bidhaa zako, kuna wateja ambao mpaka waione bidhaa mara kadhaa ndipo watakubali kutoa pesa zao, usikate tamaa kisa watu hawajachukua bidhaa zako.
Kuna wateja wengine ambao huona bidhaa na kununua hapo hapo. Jitahidi uyafahamu hayo.
Edius Katamugora
#KijanaWaMaarifa
0764145476
ekatamugora@gmail.com
#KijanaWaMaarifa
0764145476
ekatamugora@gmail.com
0 comments:
Post a Comment