Wednesday, 27 March 2019

Tutafakari Pamoja Asubuhi Ya Leo

Kila siku unapoamka tenga muda na tafakari, ni mambo gani umefanikiwa kuyafanya na ni mambo gani ulipanga kuyafanya lakini bado haujaanza kuyafanyia kazi.

           


Anza taratibu kuyafanyia kazi mambo ambayo bado haujaanza kuyafanya.

Weka malengo madogo ili uweze kufikia lengo lako kubwa.

Usidharau hatua ndogo ndogo kwani ndizo huleta matokeo makubwa, kumbuka mlango huzunguka kwenye pata ndogo. Ili upate vitu vikubwa lazima ufanye vitu vidogo mara nyingi mfululizo.

Amua leo kuanza kuchukua hatua. Fikiria ni Jumatano ngapi zimepita toka uanze kusema nitaanza wiki ijayo. Kila muda ni muda sahihi wa kuanza.

Tumia vizuri muda ulionao. Komboa muda. Wanasema muda ni pesa lakini muda ni zaidi ya pesa kwa watu wanaotumia mboni ya jicho la tatu. Unaweza kupoteza pesa ikarudi, lakini muda ukienda haurudi, kiendacho kwa mganga hakirudi. Muda ukipita umepita.

"Ukiua muda, umezika fursa," inatukumbusha methali ya kiafrika.

Asilimia tano ya watu ambao wamefanikiwa hufanya mambo ambayo asilimia 95 hawayafanyi. Unataka kuwa kati ya asilimia 5 ya watu waliofanikiwa? Anza leo kuchukua hatua. Fanya mambo tofauti usifanye kama kila mtu anavyofanya.

COME AND SEE

Edius Katamugora
Kijana WA Maarifa
0764145476
ekatamugora@gmail.com

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: