Wednesday, 17 April 2019

Somo Muhimu Toka Kwa Thomas Edson


Mmojawapo wa watu waliobaki kuishangaza dunia hadi leo hii ni Bwana Thomas Edson.

Akiwa katika mojawapo ya madarasa ya chini kabisa siku moja mwalimu wake alimuandikia barua iliyosomeka hivi, "Mwanao hawezi kujifunza, hajui kusoma na hawezi kufaulu." Mama yake baada ya kusoma ujumbe ule alijibu, "mwanangu hawezi kujifunza, nitamfundisha mwenyewe."

Ni huyu huyu Edson Thomas ambaye amekuja kuishangaza dunia. Ni mtu anayetajwa kufanya gunduzi nyingi zaidi ya mtu yeyote, amegundua mambo 1093.

Baada ya miaka 50 ya wanasayansi kuhangaika wakitaka kutengeneza taa ya umeme(light bulb) yeye aliweza kuitengeneza ndani ya miaka 3. Jaribio alilofanikisha baada ya kufanya makosa zaidi ya elfu kumi, ndipo akagundua balbu, anasema kila alipokosea ilikuwa ni njia iliyompelekea kushinda. Aligundua njia elfu kumi zizizofanya kazi.

Kwa miaka 65 mfululizo alikuwa akigundua kitu kisichopungua kimoja. Anasema, "Watu wengi wanaokata tamaa ni wale waliobakiza hatua chache kufikia ushindi." Ni marufuku kukata tamaa.

Mwaka 1964 Desemba, alipokuwa na umri wa miaka 67, alipoteza kiwanda chake kilichokuwa na thamani ya mamilioni ya kimarekani. Kilikuwa na ukubwa wa viwanja vitatu vya mpira wa miguu. Kiwanda hicho kilichokuwa kimejengwa eneo la West Orange, New Jersay kiliteketea kwa moto. Vitu vyote alivyokuwa amegundua viliteketea katika maabara yake aliyoipenda mno.

Akiwa nje akitaza moto unaoteketeza maabara hiyo, aliwaambia watoto waliokuwa wakitazama moto ule, "Watoto nendeni mkawalete mama zetu, hawatawahi kuona moto kama huu."

Baadaye akasema, "kuna Kitu kikubwa katika misukosuko. Makosa yetu yote yamechomwa. Tumshukuru Mungu tunaweza kuabza upya." Kilichofuata kama wanavyosema ni historia, baada ya wiki tatu huyu jamaa aligundua kamera.

Inawezekana ungekuwa Edson Thomas ungesema mimi ni mzee siwezi tena kufanya kitu, sikia rafiki yangu umri ni namba kisiwe kigezo cha wewe kukata tamaa, unaweza kufanya jambo lolote kubwa kama kweli una nia ya dhati.

Maisha ya Edson ni maisha yaliyojaa kukatishwa tamaa lakini hakuwahi kukata tamaa.

Umefeli mtihani, nafasi bado ipo unaweza kufaulu tena.

Umefukuzwa kazi, unaweza kupata kazi bora zaidi ya iliyopita.

Umesalitiwa au umeachwa, unaweza kupata mpenzi bora zaidi ya yule uliyekuwa naye. Acha kusononeka, smile, haumiliki matatizo yote duniani.

Maisha yako yamejaa changamoto, kumbuka maisha bila changamoto hayanogi.

Kikubwa ni mtazamo. Kuwa na mtazamo chanya siku zote.

Edius Katamugora
0764145475
ekatamugora@gmail.com

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: