Sunday 3 May 2020

CHUJIO LA 'ILI IWEJE.'



Intaneti imejaa watu wengi intaneti imejazwa vitu vingi na watu mbambalimbali.

Ni wazi kwamba unapoona kitu au kufikiria kitu unatamani ukiweke mtandaoni.



Ninaandika haya katika kipindi hichi cha korona ambapo watu wengi wakipata habari za korona wanataka wawe wa kwanza kuziweka status au kutuma kwenye magroup yao. Inawezekana kwako wewe unaona ni jambo zuri au la. 

Siongelei habari za korona tu kuna mambo mengi tunaweka mtandaoni lakini yaharibu taswira zote.

Kabla ya kuweka kitu mtandaoni kuna jaribio anatakiwa kulifanya. Jaribio lenyewe ni kupitia kujiuliza swali hili, "NAWEKA KITU HIKI MTANDAONI ILI IWEJE?" "SO WHAT?"

Je kuna watu wataelimika, je picha yangu itaonekanaje? Hakikisha kabla haujaweka kitu mtandaoni jiulize, "Nafanya kitu hiki ili iweje?"

Kama unaona kitu hakina haraka subiri saa 24 zipite ili kupisha muda wa tafakari kwa unachokifanya.



Mwandishi KEVIN KELLY anasema, "Intaneti ni mashine ya kukopi." Je upo tayari unayoyaandika watu wayashirikishe kwa wengine bila kuharibu picha yako. Hii inaambatana na yote yanayowekwa mtandaoni.

Naye Lauren Cerand anatoa njia nzuri ya kufanya jaribio hili yeye anasema, "Post kana kwa mtu yeyote anaweza kukufukuza kazi." Fikiria yote unayoyaweka mtandaoni yanatazamwa na bosi wako. Je atayapenda?

Edius Katamugora
Content Creator
0764145476
#MhandisiMwandishi

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: