Sunday, 3 May 2020

ELIMIKA NA EDIUS (3)

Ifahamu Bendi Kutoka Jalalani
________________________________________________________________

Profesa Kabudi aliwahi kusema alitolewa jalalani. Alikuwa anatania huo ni mzaha. Kuna watu wametoka jalalani yeye akasome.
Umewahi kusikia bendi kutoka jalalani? Twende pamoja👇🏾👇🏾



Huko Amerika ya Kusini, nchini Paraguay kuna kijiji kimoja kijulikanacho kama Cateura. Hii ni sehemu ambayo ni kama uswazi, ningekuwa Kenya basi mahali hapo ni kama Kibera. Cateura imezungukwa na jalala kubwa Sana.

Kila kona katika kijiji cha Cateura ni uchafu tu umezagaa. Hapa kuna familia takribani 2500  ambazo hutegemea kuchukua taka jalalani na kwenda kuziuza na wengine kupata chakula hapo. Elimu ya huko hiko chini, hakuna anayefikiria kuhusu fyucha.

Kila kona katika kijiji cha Cateura ni uchafu tu umezagaa. Hapa kuna familia takribani 2500  ambazo hutegemea kuchukua taka jalalani na kwenda kuziuza na wengine kupata chakula hapo. Elimu ya huko hiko chini, hakuna anayefikiria kuhusu fyucha.

Ripoti ya mwaka 2010 ya UNICEF kuhusu Cateura inasema takribani takribani tani 1500 za taka hutupwa katika eneo hilo.Watu wengi wasomi katika eneo hilo.



Watoto wa Cateura ndio hukusanya takataka katika eneo hilo na kwenda kuziuza. Maji katika eneo hilo si salama kabisa, siku za mvua mji hufurikwa maji yaliyochafuka yenye vijidudu na bakteria.

Siku moja Favio Chavez, mtaalamu wa mazingira alikuwa na wazo la kushangaza, wazo la kuwapa watoto kitu ambacho hawawezi kukipata.



Kitu hicho ni kucheza mziki kwenye bendi. Ingawa alikuwa amefundishwa kama mwanamuziki na alikuwa amewahi kuanzisha kikundi cha muziki alijua kwamba hakuna hata familia moja ambayo ingeweza kumudu kununua vifaa vya muziki.

Ambapo hata tarumbeta lina thamani zaidi ya nyumba. Baada ya kukaa na kufikiri aligundua kwamba suluhisho lipo ndani ya mikono yake.

Jalala lile lilikuwa na vitu vingi ambavyo vingeweza kutumika u kutengeneza vifaa vya muziki. Hivyo kutoka katika dampo hilo waliweza kutengeneza ngoma, gitaa, tarumbeta n.k


"Siku moja nilianza kuwafundisha muziki watoto wanaookota taka jalalani nikitumia vifaa vyangu," Anasema Chavez.

"Lakini nilifikia hatua wanafunzi wakawa wengi ndipo nilipoamua na kujaribu kuanza kutumia wachache." Hapo ndipo alikuwa na nguvu za kusema, "Dunia inapotutumia takataka, sisi tunairudishia muziki."

Huo ndio ukawa mwanzo wa kutengeneza bendi kutoka jalalani. Leo hii bendi hiyo inao watumbuizaji wapatao 30, wakizunguka kutoa burudani katika nchi za Argentina, Brazil na Ujerumani.



"Nilitengeneza bendi hii kuifundisha dunia na kuongeza uelewa lakini pia ujumbe kwa jamii kwamba ingawaje wanafunzi hawa wapo katika umaskini wa kutupwa, wanaweza kuchangia kitu katika jamii. Wao pia wanahitaji fursa." Anamalizia maneno hayo muasisi wa bendi hiyo Bwana Favio Chavez.

Funzo: Chimba dhahabu mahali ulipo. Unaweza kuwa unaona majani ni ya kijani kwenye upande mwingine kumbe ni makavu. "Kuzaliwa maskini sio kosa lako, kosa ni kufa maskini." (Bill Gates)
~MWISHO
#ElimikaNaEdius

Edius Katamugora
Content Creator
Creative Writer
0764145476

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: