Friday, 1 May 2020

ELIMIKA NA EDIUS (2)


_________________________________________________________________________________________

Wakati wa mauaji ya kimbali nchini Rwanda. Immaculee Ilibagiza alipoteza familia yake, baba, mama na kaka zake wawili waliouliwa na wanajeshi wa kihutu. Familia yake nzima iliuliwa kikatili isipokuwa kaka yake mkubwa aliyeitwa Aimable aliyekuwa masomoni nchini Senegal kipindi hicho.

Wakati vita imeanza alikwenda kujificha kwa mchungaji mmoja mwenye asili ya kihutu.

Mchungaji aliwaficha yeye pamoja na wanawake wenzake 7 katika bafu yenye vipimo vya mita 0.91 kwa 1.2, walikaa huko jumla ya siku 91.


Katika siku 91 alizokuwepo mafichoni siku zote alikuwa akisali. Alipokuwa akisali sala  ya BABA YETU na kufika sehemu isemayo, "Utusamehe makosa yetu Kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea," alishindwa kutamka maneno hayo kwani alikuwa na chuki dhidi ya wauaji.

Baada ya vita kuisha siku moja alikaa na kutafakari, "Kama namuomba Mungu kuniokoa katika chumba hiki nilichopo kwanini nisiwasamehe walionikosea?"

Immaculee Ilibagiza aliamua kuwasamehe walioipoteza familia yake.

Funzo: Jifunze kusamehe . Msamaha unaponya. Msamaha sio kwa ajili ya wengine ni kwa ajili yako.

#ElimikaNaEdius
#Kijanawamaarifa

Edius Katamugora
Content Creator
0764145476

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: