Monday 11 May 2020

ELIMIKA NA EDIUS (7)

ELIMIKA NA EDIUS (7)

Stori inahusu ukuaji wa taifa la mafundi mchundo (technicians) na mainjinia wa kompyuta.
__________________________________________________

1800s

Watu walikuwa wanajifunza kuunda kompyuta.

Baadhi ya wanasayansi na wanafunzi wa vyuo wakaandika mapepa ambayo yangesaidia kutengeneza kompyuta.

Sababu ilikuwa ni kwamba enzi hizo vifaa vilikuwa hakuna.


1900s

Wanafunzi wa enzi hizi wakawa  wanacheki mapepa yale wanayapitia wakaanza kuunda kompyuta ya kwanza duniani.

Likompyuta walilotengeneza ni likubwa kichizi kama Dh ya shuleni kwetu Kahororo๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ (Tazama pichani) yaani zile hosteli za Magufuli ungetoamo kompyuta Kama 6 hivi just imagine.

Yaani ukiandika 1+1 jibu unasubiri hadi kesho.

1990
Kompyuta zikawa ndogo hadi zikaanza kutumika maofisini, kwenye mabenki na kila sehemu nyeti ya nchi zilizoendelea.

Kompyuta ndo zikawa zinatumika kuendesha kazi zote za nchi kubwa.

Wakina Microsoft, PayPal, Google,  Amazon, Apple, HP na EBay.

Wakawa wanapiga hela.

1998
(USA๐Ÿ‡บ๐Ÿ‡ธ)
Kuna mwanachuo wa IT alienda zake library kusoma.

Akakuta zile pepa za watu wa 1800 walioitabiria kompyuta.

Maana walichokiandika chote ndo kilikuwa kinatumika kuunda kompyuta zote za dunia ya 1998.

Mwamba akaendelea kusoma akagundua kitu kimoja(mind you sio soma soma huyu kwamba anasoma akajibu mitihani) kuna kasoro kubwa haikuwekwa maanani..

Yaani dogo akasema, "Duh! Huu mzigo hakuna atakayepona."
(Alisema kwa kingereza lol๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ)

Dogo akakimbia kuwaambia maprofesa... Maprofesa wakaona dogo anazingua (hapa alikuwa kama yule mchizi wa 3 idiots)

Wakaamua kuhakiki wenyewe

Wakakuta ni kweli kudadeki.

Yaani BALAA ZITOOOO

1998๐Ÿ‡บ๐Ÿ‡ธ
Dogo alichogundua ni kwamba kompyuta hazikuundwa kumudu sifuri tatu (000)

Halafu mwaka 2000 ndo ulikuwa unatimba kesho kutwa hapo.

1998๐Ÿ‡บ๐Ÿ‡ธ
Basi maprofesa wakati sahihi pepa ya huyo mwanafunzi.
Mzigo ukapelekwa kwa akina Amazon, Google, Microsoft na PayPal.

Mzigo ukaenda hadi serikalini na dunia nzima.
Kila mtu akausoma.


1998
(US)
Wale wa conspiracy theory waliona wakasema, "Freemason walipanga."

Watu wa dini wakasema, "Ni mwisho wa dunia."

CNN na BBC waliona wakasema ni Y2K.

1998 (US)
Wataalamu wa programming wakaliona wakaanza kufanya majaribio.

Wakaona ikifika 2000 kompyuta zote zitasoma "1"

Basi ndege, simu, serikali, mabenki na kiiiiiila kitu chenye kompyuta kitazima na kitaleta balaa.

1998
(Uganda)

Mchungaji mmoja anaitwa Kibwetere waumini wake 1000 kuwa,

"kuanzia mwaka 2000 utakuwa ni muhula wa shetani, freemason watakuwa wanaanza kazi zao za kutawala dunia, vita na kuendesha akili za watu na 666 itakuja."

Ushahidi ni badala ya kompyuta zote kusoma "2000" zitasoma "1".

1998๐Ÿ‡บ๐Ÿ‡ธ
Wakaunda kamati ya kazi kutatua hili tatizo maana ikifika mwaka 2000 hakuna mtu atakuwa salama wakasema hata wasiite 2000 bali iitwe Y2K 
Yaani

Year 2 × 1000 = Year 2000


๐Ÿ‡บ๐Ÿ‡ธ
Serikali kushirikiana na programmers na makampuni makubwa wakapiga hesabu wakasema,

Hata tufanyeje hii nchi haina programmers wa kushato (sorry kutosha) kutatua hili tatizo.

Tufanye nini?

1999๐Ÿ‡บ๐Ÿ‡ธ
Wakaona nchi zote zinazoendelea zina uhaba wa maprograma maana wanahitajika nchini kwao,

Nchi zote zina uhaba kasoro nchi moja tu.

Rais Bill Clinton akachukua simu akawavutia waya..

1999๐Ÿ‡บ๐Ÿ‡ธ
Bill Clinton akapiga simu India.

Akamwambia rais wa India.

"Tunaombeni programmers wenu, wowote mlionao kwa bei yoyote ile tutawakatia VISA na kuwapa uraia. Tusaidieni mazee. Meli inazama (kwa sauti ya Elisante akiwa anaomba bondi)


1999
๐Ÿ‡ฎ๐Ÿ‡ณ
Rais wa India akasema,

"Wanachuo wote na hata yule anayesoma tuisheni ya programming anahitajika Marekani chap kwa haraka.

Passport + Visa unapewa getini yaaani..


๐Ÿ‡ฎ๐Ÿ‡ณ
India watu wengi balaa halafu hakuna ajira. So.

Watu walijiandikisha wengi kichizi, hata mtu aliyejua Microsoft word alijiandikisha kusepa kwenda US. Wamba wakaanza kujiiona kama Jay Z.(Kimoyomoyo wanajisemea "Silicon Valley si ndiyo hii mzee baba. Mungu atupe nini."

2000
It went fine 
All was well.

India saved the world.

Na hadi sasa hivi wahindi wapo kwenye makapuni makubwa wanafanya kazi. Unaambiwa 75% ya wafanyakazi wa Microsoft ni wahindi. CEO wa Google, Microsoft, na Adobe ni Wahindi.

Funzo: Mlango wa fursa hauna alama ya "VUTA" au "SUKUMA."

Credit to my IT Geek my brother Nicholaus Legnard (Nickyrabit)

#ElimikaNaEdius

Edius Katamugora
Content Creator
Creative Writer
0764145476
ekatamugora@gmail.com

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: