Friday 15 May 2020

ELIMIKA NA EDIUS (9)



Tegla Lorope Ni Mwanariadha aliyezaliwa Katika Familia ya watoto 24, Familia yake Ilikataa Kumpeleka Shule Akajipeleka mwenyewe
____________________________________________________
Anaitwa Tegla Loroupe alizaliwa katika kijiji kimoja huko Kenya.



Baba yake alikuwa na wake 4 hivyo Tegla alikuwa na jumla ya ndugu 24. Haujawahi kutana na watu masikini wewe!

Akiwa na miaka mitano alichohitaji ni kwenda shule lakini wazee wa kijiji kile pamoja na wazazi wake hakuna aliyetaka kumpeleka shule iliyokuwa karibu, kilomita 10 toka kwao.

 Lakini alisikia kuhusu shule na alinuia kwenda shule.

Hivyo asubuhi moja, badala ya kuchunga mbuzi alizotakiwa kuchunga, akajiseme "Potelea pote,"Tegla alikwenda na kujiandikisha shuleni (Km 10 toka kwao). 

Kulikuwa na sheria kali nchini Kenya kwamba mtoto akishaandikishwa shuleni hapaswi kukosa hata siku moja. 

Muda huo nusu mwaka ulikuwa ushakata, lakini alifika shuleni kila siku kwa kutembea miguu peku(Km 10 nakukumbusha) kwenye milima na mabonde ya Kenya, kila siku asubuhi na jioni.
Aliweza kumudu masomo yake na kufaulu darasa la kwanza.

Kitu cha muhimu ni pale yeye na watoto toka kijijini kwao walipokimbia kwenda shuleni, binti huyu alikuwa mwenye mbio zaidi hata ya wale waliomzidi umri.


Hapo ndipo akagundua kipaji chake cha kukimbia.

Miaka ya baadae alikataliwa na tume ya Ukimbia ya Kenya kuwa mmoja wa wanariadha wa Kenya kwasababu eti alikuwa na mwili mdogo.

Baadae mwaka 1994 alivunja rekodi ya kuwa mwafrika wa Kwanza wa kike kushinda mashindano ya mbio ya New York, mwaka uliofuata akashinda tena. Alipata kuvunja rekodi 3 za dunia kwenye ukimbiaji wa mbio ndefu.

Amejenga pia shule kwao Kenya na ni mmojawapo wa mabalozi wa UN wanatetea haki na amani duniani.

Funzo: Unaweza kubadili maumivu kuwa stori inayovutia siku za mbeleni. Kila unapotafakari umetoka katika familia maskini mkumbuke Tegla Loroupe aliyezaliwa familia ya ndugu 24.

Na Edius Katamugora
Content Creator 
Creative Writer
0764145476
ekatamugora@gmail.com

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: