Leo tutakua na darasa muhimu mno hasa katika kipindi hiki ambacho tunatumia mitandao kwa wingi kufanikisha mambo yetu hasa biashara. Binafsi nimekua mfuatiliaji na mtumiaji mzuri wa mitandao. Kila kukicha najitahidi kujua kitu fulani na dunia inakwenda wapi katika matumizi ya mitandao. Nimekua nikifuatilia Makosa tunayofanya mtandaoni Kama wafanyabiashara na wajasiriamali, kiukweli Ni mengi lakini leo nitazungumzia Makosa makubwa 8 yanayofanywa na watu wengi. Kwanza kabisa nianze na utangulizi. Nafahamu wengi tumekua tukitumia mitandao na tumeona faida zake tofauti na biashara zile zinazosubiri wateja. Inawezekana unajua au hujui lakini takwimu zinasema kwamba *Zaidi ya 70% ya wateja hufanya maamuzi ya kununua kitu/vitu mtandaoni. Mtu anapokuja dukani kwako au anapofuata huduma tayari anajua anataka Nini Nafikiri tukifahamu hiki kitu tutakua makini na jinsi tunavyoitumia mitandao yetu. Sasa baada ya kusema hayo niende moja kwa moja kwenye Makosa tunayofanya Makosa Wanayofanya Wajasiriamali Mtandaoni na Namna ya Kuyaepuka* 🏾🏾🏾 📩 1. Tangazo lisilo na caption (maneno kwa chini) Wengi tumekua tukiwaachia watu wa graphics watengeneze tangazo na Kisha sisi tunakuja kuweka status WhatsApp au Instagram bila kuandika chochote. Bila kuongeza chochote. Haya Ni Makosa makubwa. Tunayafanya hata kwenye matangazo tunayoshea kila siku humu. Hakikisha kila unapoweka tangazo lako kwenye mitandao ya kijamii unaambatanisha na maneno Fulani hivi mazuri ya kumvutia mteja. Weka hata sifa za bidhaa hiyo. Usiache mteja ajipe majibu kichwani. Hii huongeza hamasa ya mtu kununua. Muda mwingine wengine wanatuma picha Nyingi kwenye makundi ya WhatsApp bila kuandika chochote. Anasubiri wateja waje kuuliza. Haya Ni Makosa pia. Wakati namalizia kuandika hii makala nikakutana na maneno ya rafiki yangu Mwl.Benjamin Madaha aliyeandika hivi, "Kuposti bidhaa mtandaoni bila kuandika maneno yoyote ni kama kuweka bidhaa sokoni na ukaziacha kabisa ukifikiri zitajiuza zenyewe." 📩 2. Kutotoa thamani. Hii imesemwa mara nyingi na Mimi nimeisema Sana. Watu hununua thamani, na watu hununua kwa watu wanaowaamini na kuwakubali. Njia pekee ya watu kukuamini na kukubali ni kutoa thamani. Kama unauza nguo waeleze watu nguo Bora Ni zipi. Kisha waambie nguo Kama hizo wanaweza kuzipata dukani kwako. Unauza viatu. Wape watu hata tips za mfano: Fahamu nchi 5 Bora kwa utengenezaji wa viatu duniani. Utaeleza Kisha waambie viatu hivyo unavyo. Unatoa thamani hapo kumbuka. Unauza wigs, Wafundishe watu Namna ya kutunza mawigi yao muda mrefu.* Listi Ni ndefu. Kisha watangazie watu mawigi mazuri yanayodumu dukani yanapatikana dukani kwako. Ipo hivi: Watu wote walionunua drili hawakutaka kununua drili, walitaka kuchimba shimo, Wafundishe watu kuchimba mashimo watakuja kununua drili.* 📩3. Kukosa OFA Kuna watu humu toka wameanza biashara hawajawahi kutoa ofa. Ipo hivi Ofa sio kitu rahisi cha mteja kukataa. Ofa huleta wateja wengi kama ulikua hujui. Jitahidi siku moja moja hutoe ofa kwa wateja wako. Hii inakutengenezea ukaribu na wateja. Fikiria kwanini makampuni makubwa yanatoa ofa? Wengine ushindani ukiwa mkubwa ndipo wanatoa ofa pia hizi pia Ni Siri za kupata masoko. Hizi Pepsi Big na Coca bila sukari Ni njia za kutoa ofa. Kwamfano Ukinunua Mirinda nyeusi ya buku unakuta wameandika 20% ya nyongeza. Hiyo ni ofa. Usijione mjasiriamali mdogo toa ofa siku mojamoja. "Fanya biashara kana kwamba unashindana na kampuni kubwa." Anashauri Mark Cuban mtaalamu wa maswala ya biashara. 📩 4. Kutumia mtandao mmoja Wengine akiona anapata wateja WhatsApp tu basi anakomaa na WhatsApp tu. Ni muhimu Sana kuwa na mitandao mingi kwani wateja wanapatikana kwingi. Kuwa Instagram, Twitter, WhatsApp, Facebook na hata LinkedIn. Wengi humu tunategemea status Kama sehemu ya kukuza au kutangaza biashara zetu lakini, Siku za mbeleni WhatsApp itakua na Ads, Kama ilivyo YouTube hivyo hata watu hawatakua na muda wa kutazama status tena labda uwe na vitu vya kipekee. Hii ni Siri nimewaibia. Tujipange. 📩 5. Kukwepa matangazo ya kulipia (Sponsored Ads) Zamani njia ya kutangaza ilikua kupitia redio, magazeti na televisheni. Sikuhizi njia rahisi na ya Bei rahisi na inayoweza kukifikisha mbele ya wateja wengi Ni kupitia matangazo ya kulipia (Sponsored Ads) kupitia mitandao ya kijamii kama vile facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Wengi njia hii tumekua tukiikwepa. Tunasahau kwamba unapoweka tangazo la biashara Mtandaoni Kuna Namna Fulani Facebook na Instagram wanayozuia yasikife mbele za watu. Ndiyo maana matangazo ya biashara huwa na LIKES chache. Watu wengi wanashindwa kutumia hizi sponsored Ads lakini Ni njia rahisi. Ukipata nafasi jifunze. Unaweza kulipia Mpesa kwa njia ya LIPA KWA. Kampuni ya Coca-Cola mwaka Jana ilitumia dola bilioni 4.24 za Kimarekani kufanya matangazo. Tusione makampuni makubwa yanaendelea, watu wamewekeza mno kwenye matangazo. 📩 6. Kutojibu Maswali ya watu Kuna Maswali huwa watu wanauliza lakini hatuyajibu tunayaacha. Mwingine akija baada ya wiki kadhaa anakuta haujajibu unaonekana Kama haupo makini na bisahara yako. Jitahidi kujibu Maswali ya watu kadri uwezavyo. Hii inakutengenezea ukaribu na wateja. Kwa mfano unakuta mtu kauliza bei gani na hajibiwi, uzembe kama huu unaweza poteza wateja. 7.7. 📩 Matumizi ya Shuhuda (testimonies) Umewahi kuona mtu ameombewa na anatoa ushuhuda alivyoponywa? Ni kitu gani huwa kinakujia kichwani? Kama ulikua na tatizo Kama lake utahitaji nawe uombewe. Hii kwenye biashara ipo pia. Watu wa biashara ya mtandao (network marketing) wanaweza sana hii kitu, atakuonesha mtu alikua mnene (kibonge) baada ya kutumia bidhaa zao amekuwa mwembamba. Mteja anaposema kitu kizuri kuhusu bidhaa yako, screenshot uweke mitandaoni. Hii inavuta wateja wengine zaidi. Wengi humu mnaishia kusema "Asante" 🏾MAKOSA MAKUBWA 8. 📩 Kutotumia Watu wenye Ushawishi Kunadi biashara zetu Kuna watu Ni mashuhuri na Kuna watu wenye Ushawishi (Influencers) unaambiwa vijana wengi Sasa hivi wanawasilikiza hawa watu kuliko hata wazazi wao. Ukiwatumia watu hawa kutangaza bidhaa au huduma yako Ni rahisi kupata wateja kuliko hata wewe. Kumbuka Tena Watu hununua kwa watu wanaowapenda na wanaowaamini. Sasa Kama watu wanamkubali Influencer Fulani anayeuza au tangaza bidhaa yako kwanini wasinunue kitu anachouza? Tutumie watu wenye Ushawishi kutangaza bidhaa zetu. Faida kubwa waliyonayo watu hawa ni kwamba hawatozi gharama kubwa. Ni Namna mnavyokubaliana. Na Edius Katamugora ekatamugora@gmail.com 0764145476
|
0 comments:
Post a Comment