Tuesday, 13 October 2020

MAMBO AMBAYO PRINCESS HATAKIWI KUFANYA

 



Mabinti wengi hata wanawake waliokwisha enda umri huwa wanatamani nao wangekuwa MaPrincess. Huwa wanafikiri kuwa Princess unalelewa kama yai.

Kuna wapuuzi wawili ndo Kwanza wana penzi la wiki moja tayari wanaitana Prince na Princess. Unamuita mtoto wa mtu Princess unajua Princess Ni mtu wa namna gani wewe? Haya sasa ngoja nikupe kashkash anazokumbana nazo princess.

Twende wote

Moja Princess lazima ajue kuongea lugha nyingi Sana. Hii ni kwasababu anatakuna na wanadiplomasia wengi. Hivyo lazima awasiliane nao.

Pili, kuwa Princess tu kibali au haki ya kupiga kura haipo kwako tena, kura utazisikia kwa wajumbe. Sio Mimi jamani Ni sheria.

Tatu, kuwa Princess utakiwi kuwa mpuuzi mpuuzi, sijui leo una skendo au msumbufu. Thubutu! Maana unaiwakilisha Royal Family.

Nne, Princess Hana A.K.A wala Nini. Sasa wewe huku kitaa unaitwa Anna ila insta unajiita Precious mara Sweet Manka, kwa Princess hakuna kitu Kama hicho.

Tano, Princess lazima avalie vizuri muda wote, kudamshi ni lazima Sio ombi.

Sita, lazima afuate sheria zote anazotoa malkia. Atake asitake.

Saba, lazima aende vyuo Bora na aende kwenye tafrija za kibabe. Huji kumkuta Princess anasoma Zion neva! Harusi anaudhuria zile za kishua tu.

Nane, kuwa Princess Ni kazi tayari uruhusiwi kuwa na kazi nyingine yoyote.

Tisa, Kucha zake lazima zipakwe vitu vya asili (natural) hapaki marangi Wala kubandika kucha, wadada mpo?

Kumi, Princess hapaswi kuwa kwenye mitandao ya kijamii. Kama unasoma ujumbe huu kupitia mtandao wowote wa kijamii, tayari hii Ni total disqualification.

Imeandikwa Nami;
Edius Katamugora
Content Creator

Unaweza kupata VOLUME 1 ya kitabu chenye stori za ELIMIKA NA EDIUS kwa bei ya ofa ya 2000/= tu lipia kwenda 0764145476 kisha utatumiwa kitabu chap kupitia WhatsApp au email.

 



Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: