Thursday 16 July 2020

USIKUBALI KUMALIZA CHUO BILA AINA 4 HIZI ZA UJUZI

Kazi kubwa ya vyuo vikuu ni kuwaonesha wanafunzi wake ni vitabu gani wasome. Ukweli ni kwamba wanavyuo wengi wanaweza kupata maarifa kwa kujifunza wao wenyewe. Kitu kibaya tulichonacho katika vyuo vyetu vingi hapa nchini unakuta mwalimu anakitabu chake maalumu anaficha ili wanafunzi wake wasijue anatoa wapi notisi. Hii ni mbaya sana na inaharibu namna ya kusambaza maarifa. Mwalimu anafurahia akikamata watu wengi. Inasikitisikitisha.



Nakumbuka mwaka 2017 nilisoma kitabu kimoja cha Peter Drucker gwiji wa mambo ya manejimenti (jina la kitabu sikumbuki vizuri). Anasema, mwalimu bora ni yule anayetumia kitabu/vitabu kufundisha wanafunzi wake.

Lakini pia kazi kubwa ya Vyuo ni kuwafundisha watu ujuzi mbalimbali.(Kama ni mwanachuo na haujapata haya chuoni tafuta muda wako na ujifunze. )

Aina mbalimbali za ujuzi ambao vyuo vinapaswa kuutoa๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ

1. Ujuzi wa taarifa: Namna ya kupata taarifa kutoka vyanzo mbalimbali, ikihusisha vyanzo vya kidigitali(intaneti), vitabu na kutoka kwa stafu(walimu.)

2. Ujuzi wa kufikiri. Dunia inaongozwa na wanaofikiri. "Katika nchi ya waliofanikiwa watu hawapimwi kwa urefu au ufupi wao wala rangi zao bali kwa kiwango chao cha kufikiri." (David Schwartz). Hapana nazungumzia tafakari tunduizi ( critical thinking), kufikiri kibunifu, kujenga fikra, n.k Daima kumbuka mambo mengi makubwa ni matokeo ya mawazo yaliyotoka kichwani. "Wale wanaofikiri ni vichaa kiasi cha kufikiri wanaweza kuibadili dunia ndio wanaoweza," aliwahi kusema mwanzilishi wa Apple Inc Steve Jobs.

3. Ujuzi wa watu (People Skills). Hapa utajifunza namna ya kudili na watu, namna ya kuwaongoza watu, kuwaelewa watu, n.k. Somo letu la juzi kuhusu Kutengeneza mtandao hapa ndipo linafanyiwa kazi. Nakushauri usome kitabu cha Dale Carnegie kinaitwa How To Win Friends and Influence People, kuna nondo nyingi utajifunza au Never eat Alone cha Keith Ferazzi utajifunza mengi kuhusu watu au soma kuhusu saikolojia mbalimbali za watu.



4.Ujuzi wa kitaalamu: Hapa unatafuta ujuzi unaoendana na kitu unachosomea au uwanja uliopo. Wengi wanatafuta hii kitu na wanasahau hizo mbili nilizoanza nazo. Kumbuka kwamba sikuhizi kazi ni ngumu kupata ukiwa una ujuzi 1-3 niliosema unaweza kufanya chochote huku ukiangalia kufanya kazi ya kitu ulichosomea.

Mwisho
Imeandaliwa na
Edius Katamugora
ekatamugora@gmail.com
0764145476

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

2 comments:

Unknown said...

Ahsante sana Kaka Kwa maarifa.nazikubali kazi zako keep inspiring the young generation








Edius Katamugora said...

Karibu sana