Mojawapo ya kitu kitakacho kufikisha mbali ni kuwa na mahusiano yanayoeleweka.
Sio
rahisi kukuta mtu ana wake wengi ukakuta ana maisha yaliyonyooka,
tazama hata vijana ambao unakuta kila uchao anamahusiano na mtu mpya,
akili zao ni kupata pesa za kula na kuvaa, full stop.
Hawawezi kingine, hawana malengo hawana mipango na hakuna kitu chochote cha maana wanachofanya.
Ukiwa
na mahusiano mengi lazima muda wako ufie huko, utaongea na huyu
ukimaliza utampigia huyu. Au ukimaliza kuonana na huyu utaenda kwa kwa
yule matokeo yake ni kupoteza muda Tu.
Kwenye Kitabu cha Matatizo si tatizo (Matatizo ni Daraja) Fr. Faustin Kamugisha ametoa stori ya HENRY FORD.
Henry Ford ni mwanzilshi wa kampuni ya kutengeneza magari aina ya Ford.
Akiwa anatimiza Jubilei ya miaka 25 ya ndoa yake, MC alimuuliza aseme nini Siri ya mafanikio ya ndoa yake.
Alijibu, "Siri ni ile ile ninayo tumia kwenye magari, sijawahi badili modeli ya gari."
Wewe
unabadili modeli kila siku. Unakutana na mdada mwaka mmoja tu amekuwa
kwenye mahusiano na watu 7 tofauti unajiuliza maswali hadi unakosa jibu.
Wakaka ndo usiseme, Leo anapost huyu kesho Yule, yaani vurugu mechi.
Niliandika
kwenye kitabu changu cha PUMBA ZA EDIUS "Hakuna fomula inayosema kwamba
ukitoka kwenye uhusiano mmoja unganisha na kuanza mwingine. Muda
mwingine unahitaji kuwa peke yako ujitafakari na kugundua ulifeli wapi.
Jipe muda. Sio lazima kila wakati uwe kwenye uhusiano, muda mwingine
unahitaji kuwa na uhusiano na wewe mwenyewe."
Kabla
ya kuandika kitabu chake cha THINK AND GROW RICH Napoleon Hill
aliwahoji matajiri Zaidi ya 500 ili kupata majibu ya nini kiliwafanya
wawe matajiri kuwa na mahusiano yanayoeleweka lilikuwa jibu mojawapo.
Usichukulie poa mahusiano, Yana mchango mkubwa kwenye kufanikiwa au kutofanikiwa kwako.
Imeandaliwa Na
Edius Katamugora
ekatamugora@gmail.com
0758594893 (WhatsApp)
0 comments:
Post a Comment