"Wale ambao wanafikiri ni vichaa kiasi cha kutosha, ndio wataibadili dunia" (Steve Jobs)
Kama haupo tayari kuitwa chizi au kuonekana kichaa, basi tambua kwamba mafanikio kwako ni kitendawili.
Kwenye unalolifanya watu kuna hatua hawatakuelewa.
Ngoja niwape mfano.
Wakati
naanza kuandika post za PUMBA ZA EDIUS huko Facebook, watu wengi
walinijia juu, tena wengine Kwa hasira wakisema, Edius unachafua jina
lako, mara ooh unakitu kizuri lakini umekipa jina baya.
Niliwajibu
asante. Siku moja dada mmoja akaniomba namba Facebook nikampa,
akanipigia. Akaanza kunihubiria kwamba anapenda makala zangu lakini neno
Pumba linamkera. Nikamwambia nitabadilisha, nikaendelea sikuacha
kutumia neno Pumba.
Siku nyingine akaja mtu ananiandikia waraka mrefu tena akitumia vifungu vya biblia lakini nikasoma Tu hata sikumjibu.
Nimesikia
kelele nyingi kuhusu kutumia neno PUMBA ZA EDIUS lakini ambacho wengi
hawajui ni kwamba katika vitabu vyangu vyote Pumba za Edius ndo kitabu
kimesomwa na watu zaidi ya 30000 tena kinapendwa kuliko kawaida.
Wengine wananiuliza kwamba sina kingine cha dizaini ile. Nawaambia hapana lakini wanaanipa mawazo ambayo nayafanyia kazi.
Nisingeanza na Pumba za Edius inawezekana hii Menta kama Menta isingekuepo.
Unajua
kwenye Sanaa unahitaji ubunifu, kama ukitaka kila kitu kiende kwenye
mstari, unakufa. Hakuna atakayetaka kazi zako. Binafsi naamini Sana
kwenye ubunifu na kujifunza vitu vipya.
Kama wewe ni msomaji Sana. Pumba za Edius haliwezi kuwa neno lenye ukakasi hata kidogo.
Ngoja niwape mifano kuna hivi vitabu sijui mmewahi kuvisoma?
1. The subtle art of not giving a fuck Mark Manson
2. Everything is fucked
3. Nobody wants to read your shit Steven Pressifield
Hapa Tanzania tuna waandishi wa namna hiyo tena ukisoma wanayoandika ni noma na nusu
Masoud Kipanya ana kitu anakiita Upuuzi wa Masoud
Jamhuri kuna jamaa anaandika makala anajiita Mzee zuzu
Mwananchi kuna jamaa ana makala zina jina la HEKAYA ZA MLEVI. Ukisoma ndo utajua amelewa au yuko soba.
Nimalize Kwa kusema, kuonekana umekua chizi, watu wasikuelewe ni sahihi pia kikubwa amini unachokifanya.
Kwenye
kitabu chake cha Do the Work Steven Pressifield anasema, "A Child has
no trouble believing the unbelievable, nor does the genius or the
madman. It's only you and I, with our big brains and our tiny hearts who
doubt and overthink and hesitate."
Tangazo:
Kama utahitaji kitabu cha PUMBA ZA EDIUS nicheki WhatsApp kupitia namba
0758594893 nitakutumia Bure. Tuma neno PUMBA ZA EDIUS utatumiwa kitabu.
Edius was here
ekatamugora@gmail.com |
0 comments:
Post a Comment