Wednesday 26 October 2016

Ili Hufanikiwe Lazima Huamke Muda Huu.

Habari mpendwa msomaji wa bideism blog, ni matumaini yangu kwamba unaendelea vizuri na safari ya mafanikio.
"Kulala mapema na kuamka mapema hutengeneza siku  nzuri" ni msemo wa waingereza, na "panzi anayelala kwa kujisahau huamka na kujikuta kwenye mdomo wa mjusi" ni msemo wa Waigbo wa Nigeria.
Ripoti mpya iliyoandikwa kwenye gazeti la Wall street
Inasema muda muafaka wa kuamka ni SAA Kumi alfajiri. Hili kuongeza mafanikio na uzalishaji zaidi hizi ndizo sababu za kuamka muda huo;

-Usumbufu unakuwa haupo au ni kidogo sana (kama watoto na kazi).
-Hakuna anayekutumia email au anawasiliana na wewe (chatting).
-Kuna machache tu ya kuangalia katika mitandao ya kijamii.
Kuamka muda huo utaweza kufikiri juu ya maisha yako (meditation) na itakupa nguvu siku nzima kufanya kazi ipasavyo na kushughulikia kwa makini hasa mambo ya kifamilia na kusaidia kukuza imani yako ya dini.
Tim Cook meneja/CEO wa  kampuni ya Apple
anasema "Mimi huwa naanza siku yangu SAA 9 na dakika 45 usiku".

Je wewe huwa unaamka SAA ngapi?
Muda unaoamka unakupeleka kwenye mafanikio au la?
Anza sasa kujitahidi kuamka mapema hili mambo yako yaende sawa kwani "kujaribu na kushindwa sio uzembe" ni msemo wa Sierra Leone, jaribu sasa kuanza kuamka mapema.
Nakubaliana na Stamina anayesema "unayelala endelea kulala ukiamka utakula ulichokiota".

Ni mimi rafiki yako na ndugu yako Eddy Bide
Tuwasiliane: whatsapp 0625951842
Email: ekatamugora@gmail.com
Instagram: eddybide

Endelea kusoma makala nzuri kwenye blog hii kila siku. Asante

"See you at the top".

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: