Sunday 1 January 2017

Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Bideism blog inachukua nafasi ya pekee kukupongeza kuuona mwaka mpya. 2017.

Ningependa kukualika katika mada niliyokuandalia leo hii.
Je umejiandaa?
Mpendwa msomaji tunapouanza mwaka MPYA tunaweka malengo ambayo tunategemea kuyatimiza katika mwaka huu wa 2017. Kama ujaweka malengo yako leo uchachelewa, chukua kalamu na karatasi andika umepanga kufanya nini  mawazo yakiandikwa kwenye karatasi yanakuwa na maana zaidi usiyaache kichwani.
Ukitaka kufanikiwa lazima ujiandae, mwanafunzi ili ashinde mitihani lazima ajiandae kwa kusoma kwa bidii ili aweze kufaulu. Kumbuka;

""Mvua ilikuwa hainyeshi Nuhu alipoanza kuijenga safina'' jiandae ufanikiwe.

Mwanajeshi kabla ya kwenda vitani lazima aandae siraha mathubuti zitakazo msaidia kushinda vita husika.

Mkulima pia lazima aandae shamba lake ili mvua zikianza apande mimea yake ikue kwa kushamili na apate mavuno bora. Kuna msemo unasema '' utavuna ulichopanda'' panda maandalizi mema uvune mafanikio. Mkulima hawezi kupanda magugu akitegemea kupata mahindi. Hasha.

Mwandishi wa makala naye lazima ajipange na kuaandaa ataandika nini, anayapanga Yale atakayooandika ili aeleweke ndio maana ukitembelea mtandao wa SONGAMBELE unaoendeshwa na rafiki yangu na mwanadarasa Wangu ndugu GODIUS Rweyongeza utagundua anajiandaa kuliko kawaida.

Mwaka unapoanza, wewe unayesoma makala hii umejiandaaje kupambana kufikia malengo yako uliyopanga kuyafanya. Mwandishi wa kitabu cha ''hatupangi kushindwa tunashindwa kupanga'' Dr. Faustine Kamugisha anaongelea mengi kuhusu kujiandaa na kujipanga usisite kutafuta nakala yako.

Timu unazoziona zinafanya vizuri uwanjani, azivamii tu mchezo, wanajaiandaa kwa kufanya mazoezi makali na kusoma mbinu za wapinzani wao. Utavuna ulichopanda. Panda maandalizi mema uvune mafanikio.

Nakutakia maandalizi mema katika mwaka huu tuliouanza leo wa 2017.

Ni Mimi rafiki na ndugu yenu.
Edius Katamugora
Tuwasiliane;
0764145476
Whatsapp; 0625951842(tuma neno ''SUBSCRIBE'' niwe nakutumia makala zangu).
Email;ekatamugora@gmail.com

Asante kwa kuwa na Mimi mwanzo hadi mwisho.

"See you at the top".

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: