Saturday 31 December 2016

Mafanikio Ni Kujiongeza

Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama katika siku hii ya jumamosi ambayo pia ni siku ya mwaka 2016. Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kufika mwisho wa mwaka. Ni vyema na wewe kushukuru.

Jambo ambalo ningependa kukuasa kabla ya mwaka kuanza ni kujifunza kuwa chanya. Watu hasi, matendo hasi, fikra hasi achananazo unapouanza mwaka 2017.

Karibu sana katika makala niliyokuandalia leo inayosema '' mafanikio ni kujiongeza''.
Mpendwa msoma kila mtu unayemuona kafanikiwa katika ili ama lile kuna sehemu kajiongeza, kwa kiingereza tunaweza kusema ''going extra miles''.

Zamani ulikuwa ukisafiri kwenye mabasi upewi chochote zaidi ya tiketi tu, leo hii mabasi yana TV ndani, umo unapewa vyakula na mapochopocho mbalimbali na watu wengi wamekuwa wakipenda kupanda magari hayo. Huko ndiko kujiongeza kwenyewe.

Bofya hapa kusoma: kushindwa ni vijilia ya kushinda

Ukifatilia kwa ukaribu siku hizi kwenye vituo vya mafuta watu wanaweka super market, wamejiongeza na kuona fursa yakwamba mtu akiwaanasubiri ajaziwe mafuta anaweza akanunua kinywaji chochote cha kupoza koo. Hii ndio maana halisi ya kujiongeza.

Ukiwa unafanya kitu chochote jaribu kujiongeza nakuahidi mafanikio ya hali ya juu. Leo hii tunaishi katika kizazi ambacho watu wanasoma biashara lakini hawana hata wazo lolote la biashara vichwani mwao. Kizazi ambacho tuna watu wanaosoma masomo ya IT lakini hawana hata uwezo wa kumiliki blog na kufungulia watu blog mbalimbali za biashara wanazo Fanya kwani biashara ni matangazo.

Napenda kuchukulia mfano raisi wa Marekani Bwana Donald Trump, uyu bwana ni mtu anayejiongeza sana kwa misemo ya siku hizi unaweza sema si mtu wa mchezomchezo. Trump kabla ya kuwa raisi ni mwandishi wa vitabu, mfanyabiashara mkubwa, ameshiriki kama muigizaji katika muvi nyingi tu!! Ndio usishangae kwa uthibitisho tafuta muvi inaitwa home alone utamuona kwa macho yako. Mbali na hilo Trump amewahi kuwa meneja wa mchezo wa mieleka . Ni kujiongeza kulikoje.

Bofya hapa kusoma: Tujifunze nini toka kwa Trump

Mmiliki wa Facebook bwana Mark Zurgenberg pia ni mfano wa watu waliojiongeza, pamoja na kuwa na diploma ya kompyuta aliyoipata chuo cha Harvard mwaka 2002. Tazama alivyoweza kugundua mtandao huu ambao umenfanya kuwa bilionea.

Kumbe katika na sisi tunachokifanya inabidi tujiongeze au tukifanye kwa jicho la pili. Kama ni mfanya biashara angalia ni kwa namna Fulani unaweza kuikuza biashara yako. Kama ni mwanafunzi umiza kichwa chako na kufikiri unachokisoma kitakuleteaje mafanikio. Sehemu yoyote unayofanya kazi jifunze kujiongeza, uwa napenda kusema msemo mmoja ''usifikirie tu pale chini ulipo fikiria na juu unapoweza kuwa".

Ni Mimi rafiki na ndugu yako.
Edius Bide Katamugora
Tuwasiliane:
0764145476
Whatsapp: 0625951842 (tuna neno SUBSCRIBE niwe nakutumia makala zangu)
Email; ekatamugora@gmail.com
Instagram: @eddybide

Usisite kuwashirikisha wenzako unachokipata hapa. Asante

"See you at the top".

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: